BIBI YAKE NYOTA WA BIG BROTHER AFUNGWA MIAKA MINNE JELA KWA DAWA ZA KULEVYA...

Bibi Diane Gibson (kushoto) na Josie Gibson.
Nyota wa Big Brother, Josie Gibson alikuwa mahamakani jana kushuhudia bibi yake akifungwa kwa zaidi ya miaka minne kutokana na mashitaka ya dawa za kulevya.

Mtangazaji huyo wa televisheni, ambaye alibadilisha mavazi yake kabla ya kurejea mahakamani hapo jana mchana, aliungana na wanafamilia wengine katika Mahakama ya Bristol kushuhudia Diane Gibson, mwenye umri wa miaka 72, akihukumiwa kifungo cha miaka minne na miezi mitatu jela.
Bibi huyo alikuwa mafichoni kwa zaidi ya miaka 12 baada ya kuwa ametiwa hatiani mwaka 2000 kwenye Mahakama ya Bristol kwa kupatikana na dawa za kulevya kwa lengo la kuzisambaza.
Diane alikuwa amekamatwa na polisi mwaka 1998 akiwa na kilo 2.9 za cocaine - zenye thamani ya mitaani ya Pauni za Uingereza 240,000 - ndani ya buti la gari lake.
Aliachiwa kwa dhamana akisubiria kurejea mahakamani kwa ajili ya hukumu lakini alishindwa kutokea na kujificha, akiishi kaskazini mwa Uingereza mbali na familia yake.
Polisi walimkamata mstaafu huyo Aprili mwaka huu nyumbani kwa binti yake huko Yate, South Gloucestershire, na jana alirejea mahakamani kuhukumiwa.
Akimhukumu kifungo jela bibi huyo, Jaji Geoffrey Mercer alisema: "Ninakuhukumu kwa misingi kwamba ulikuwa msambazaji wa kiwango hiki cha cocaine.
"Ninazingatia umri wako na ninakuchukulia kama mtu mzuri na ninazingatia nilichosoma kuhusu afya yako.
"Hili si zoezi rahisi la kuhukumu lakini katika hukumu yangu adhamu ndogo kabisa ambayo inastahili kwa kosa la kumiliki cocaine kwa lengo la kusambaza ni moja ya miaka minne gerezani."
Jaji huyo pia alimhukumu Diane miezi mingine mitatu gerezani kwa kosa la kutoroka na kukaa mafichoni kwa miaka 12 iliyopita.
Wakati Jaji huyo akihitimisha kesi dhidi ya Diane, mstaafu huyo alipiga mayowe kutoka kwenye kizimba: "Sijawahi kufanya hivyo."
Wanafamilia, akiwamo Josie, walipiga kelele kutoka sehemu ya wanayokaa wasikilizaji: "Asante, tunashukuru' baada ya jaji huyo kumaliza jukumu lake.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item