Jamaa kapiga magoti kuwasilisha maombi yake kwa Mungu na mambo yakawa hivi. Jamaa: "Ee Mungu baba, naomba unipatie gari kubwa na wasichana kibao pembeni yangu." Mungu: "Ni hayo tu?" Jamaa: "Ndiyo!" Baada ya siku chache jamaa akapata kazi ya kuendesha basi la shule moja ya wasichana!! Kasheshe...