CHEKA TARATIBU...

https://roztoday.blogspot.com/2013/06/cheka-taratibu_27.html
Mke kamwomba mumewe pesa ya kununulia nyama kwakuwa aliitamani sana. Mume akamshika mkono mkewe na kwenda naye hadi kwenye kioo kisha akatoa Shilingi elfu tano na kusema:
"Unaiona ile hela kwenye kioo? Ile ndio yako kaichukue!" Jioni mume aliporudi akakuta mke kapika nyama. Mume akahoji alikopata pesa. Mke akamshika mkono mumewe na kwenda naye hadi kwenye kioo kisha akasema: "Unamuona yule mwanamke kwenye kioo? Yule ndio mkeo! Mimi niliyesimama hapa ni mke wa jamaa wa buchani!" Kasheshe...