UNENE ULIOKITHIRI WAMWOKOA BIBI ASIPANDISHWE KIZIMBANI...

https://roztoday.blogspot.com/2013/06/unene-uliokithiri-wamwokoa-bibi.html
![]() |
Rita Astbury akionesha picha aliyopiga na wajukuu zake. |
Mwanamke aliyenenepeana amekwepa kupandishwa kizimbani sababu maofisa waliamua kuwa kumtoa kwenye nyumba yake ingekuwa hatari.
'Kibonge' huyo anayeshinda kitandani, Rita Astbury, mwenye miaka 56, alikuwa afikishwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Blackpool kujibu mashitaka ya kushindwa kuhakikisha mjukuu wake wa kike, aliyekuwa akimlea, anahudhuria shule.
Lakini pale maofisa kutoka mahakama hiyo walipomtembelea nyumbani kwake katika mji ulioko pembezoni mwa bahari, waliamua kwamba kumtoa nje ya nyumba yake na kumfikisha mbele ya hakimu kungeweza kusababisha hatari kwa afya yake na sababu za kiusalama.
Ofisa ukamataji David Riches, ambaye alichukua uamuzi huo, alimweleza hakimu: "Nilikuwapo nyumbani kwake na kwa kweli sasa amekuwa na umbile kubwa mno kuweza kukamatwa."
Rita, ambaye pia anakabiliwa na makosa ya kuvunja masharti ya dhamana kwa kushindwa kurejea kusikiliza kesi zake mwanzoni, alielezwa kesi hiyo imeahirishwa baada ya kuwa imeamuliwa ilikuwa hatari mno kumtoa hapo.
Bibi huyo aliyekuwa akishitakiwa kwa kushindwa kuhakikisha wajukuu zake wawili, ambao alikuwa mlezi wao kisheria, wanakwenda shule.
Makosa ya Sheria ya Dhamana yalitupiliwa mbali lakini Rita sasa anakabiliwa na uwezekano wa kuwapoteza wajukuu zake hao wa kike, wenye umri wa miaka 15 na 13, ambao ni watoto wa binti yake kabisa.
Aliteuliwa kuwa mlezi wao kisheria mwaka 2002 baada ya mama yao kuhangaika kujaribu kuendana nao.
Mwaka 2009, mama wa binti hao aliwatorosha kutoka nyumbani kwa Rita baada ya kusema alikuwa akiwapeleka kuogelea, na kuwachukua kwenda nao kuishi na mpenzi wake mpya nyumbani kwa mwanaume huyo nchini Morocco, ambako walibadilishwa dini na kuwa Waislamu.
Wasichana hao walikaa miaka mitatu wakiishi kwenye kijiji kilichojitenga nchini Morocco na kisha wakarejeshwa kwa bibi yao baada ya mapambano ya kimataifa ya umiliki.
Sasa, hatahivyo, anakabiliwa na kuwapoteza kwa nia njema huku wafanyakazi wa huduma za jamii wakifikiria iwapo anaweza kuwachunga inavyopasa.
Msemaji wa Halmashauri ya Blackpool alisema kwamba huduma za jamii walikuwa wakichukulia kesi hiyo na mabinti hao wanaweza kuondolewa kutoka kwa Rita 'kwa faida yao.'