FAMILIA YATOFAUTIANA MAHALI ATAKAPOZIKWA MZEE MANDELA...

Watu mbalimbali wakiendelea kuweka meseji za kumtakia afya njema Mzee Mandela pamoja na maua.
Suala la mahali atakakozikwa Rais wa zamani Nelson Mandela atakapofariki dunia, limesababisha tofauti ndani ya familia yake.

Hali hiyo ilibainika juzi baada ya mjukuu wake, Chifu Mandla Mandela kususa kikao cha familia hiyo na kutoka nje, akionesha kukasirishwa na mjadala wa kufukua miili ya watoto watatu wa Mandela.
Familia inataka makaburi ya watoto hao-Makgatho, Thembekile na Makaziwe – yahamishiwe Qunu ambako Mandela atazikwa.
Vyanzo vitatu vya habari vililiambia gazeti la The Star, kwamba familia hiyo ilitofautiana na Mandla ambaye anataka babu yake azikwe mahali alikozaliwa, Mvezo, huku wengine wakitaka wosia wake wa kuzikwa karibu na wanawe uheshimiwe.
The Star iliripoti kwamba kikao cha familia hiyo kilichofanyika Qunu juzi, kilikuwa ni cha kujadili masuala nyeti ya kifamilia.
Kikao hicho kilihudhuriwa na familia, kiongozi wa chama cha United Democratic Movement (UDM), Bantu Holomisa na Waziri wa Huduma za Umma na Utawala, Lindiwe Sisulu.
Nalo gazeti la The Times liliripoti, kwamba kundi la wazee lilikuwa likipanga kwenda Gauteng kufanya tathmini ya anavyoumwa Mandela na kuamua cha kufanya.
Liliripoti, kwamba mkutano wa juzi ulijielekeza zaidi katika afya ya Mandela na kuhamishwa kwa makaburi ya familia kutoka Qunu kwenda Mvezo mwaka 2011. Makaburi hayo yalihamishwa na Mandla.
The Times liliendelea kuripoti, kwamba familia ilikuwa ikitaka makaburi ya watoto watatu wa Mandela yawe Qunu.
Gazeti hilo liliripoti pia, kwamba lilielezwa kuwa Mandla ambaye ndiye alihamisha makaburi hayo bila kuwasiliana na familia alisusa kikao kwa hasira. Hata hivyo, hakuweza kupatikana kuzungumzia kadhia hiyo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item