MWANAMKE ASHINDIA SODA KWA MIAKA 16 NA KUAMBULIA MARADHI YA MOYO...

Mwanamke mwenye umri wa miaka 31 ambaye alikimbizwa hospitali kutokana na matatizo ya moyo amewafichulia madaktari kwamba alikuwa akinywa soda tu tangu alipokuwa msichana mdogo.

Mwanamke huyo, kutoka Monaco, nchini Ufaransa, alipelekwa kwenda kuonana na daktari baada ya kuanguka.
Baada ya vipimo, iligundulika kwamba alikuwa na dalili za muda mrefu za QT - hali ambayo husababisha mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.
Mgonjwa huyo, ambaye hakutajwa jina lake, hakuwa na historia yoyote ya familia kuhusu hali ya moyo - lakini alikiri kwamba hakuwahi kunywa maji tangu alipokuwa na umri wa miaka 15, badala yake alikuwa akinywa lita mbili za soda kila siku.
Alikuwa na kiwango hatari cha chini kabisa cha posassium mwili mwake. Kirutubishi hicho hufanya kazi kubwa ya kudhibiti mapigo ya moyo ya binadamu.
Baada ya kuacha soda kwa wiki moja, kiwango cha potassium katika mwili wa mwanamke huyo na mapigo ya moyo yalionekana kurejea katika kiwango cha kawaida, kwa mujibu wa ripoti ya kesi yake iliyochapishwa wiki hii.
Utafiti wa mahusiano kati ya matatizo ya moyo na unywaji soda uliopindukia umefanywa na kugundua matatizo kama hayo.
Februari, ofisi ya mkemia ilithibitisha kwamba mama mmoja wa miaka 30 mwenye watoto wanane kutoka New Zealand alifariki kwa ugonjwa wa moyo uliosababishwa na unywaji mkubwa wa soda.
Natasha Harris aliripotiwa kunywa hadi galoni 2.6 za Coca Cola kila siku, kwa mujibu wa ripoti.
Mama mmoja mwenye miaka 42 nchini Uingereza aliripotiwa kusumbuliwa na maumivu makali ya kichwa kama asipokunywa angalau glasi moja ya soda kwa saa, imeripotiwa.
Wakati huo, Jakki Ballan, kutoka Cheshire, yeye alikuwa akinywa lita 16 kwa siku, na kumgharimu takribani Dola za Marekani 4,600 kwa mwaka.
Dk Naima Zarqane wa Kituo cha Hospitali ya Princess Grace mjini Monaco, alieleza: "Jambo moja muhimu ambalo wataalamu wa moyo wanatakiwa kuzingatia ni uhusiano kati ya soda na upungufu wa potassium, na wanatakiwa kuwauliza wagonjwa wanaogundulika na urefushwaji wa QT kuhusu tabia za kupenda viburudisho."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item