MWANAFUNZI WA UDAKTARI ABAKWA NA KUNDI LA WANAUME AKITOKA KUJISOMEA...

https://roztoday.blogspot.com/2013/06/mwanafunzi-wa-udaktari-abakwa-na-kundi.html
Mwanafunzi wa udaktari mwenye miaka 22 amebakwa na kundi la wanaume watatu ambao walimnyaka kutoka eneo la chuo kikuu kimoja chenye sifa njema nchini India.
Msichana huyo alitekwa nyara kutoka Chuo Kikuu cha Manipal mjini Karnataka wakati akitembea kurejea chumbani kwake kutoka maktaba majira ya 5:45 usiku wa Alhamisi.
Wanaume watatu wanasemekana kumburuta msichana huyo na kumpeleka kwenye eneo lililojitenga ambako wanadaiwa kumbaka, kumtelekeza akiwa kavunjika mguu na mgongo na majeraha shingoni.
Mwanafunzi huyo alilazwa hospitalini kwa matibabu Alhamisi usiku na sasa anasemekana kuwa 'kwenye mikono salama'.
Msichana huyo, ambaye alirejea chuoni hapo saa za mapema Ijumaa asubuhi, alielezewa kuwa kwenye mshituko na 'hofu' baada ya tukio hilo.
Polisi walisema haikuweza kufahamika kama alirejeshwa tena chuoni hapo na washambulizi wake au aliweza kurejea mwenyewe.
Hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo, lakini mkuu wa polisi wilaya ya Udupi alisema maofisa wanaimani ya 'kuwanasa mapema' watuhumiwa hao.
Msichana huyo inaaminika kuwa ni mwenyeji wa Kerala.