NDEGE YENYE ABIRIA 218 YATUA KWA DHARURA BAADA YA TAA YA MAFUTA KUWAKA...

https://roztoday.blogspot.com/2013/06/ndege-yenye-abiria-218-yatua-kwa.html
![]() |
Chumba cha marubani. |
Ndege Boeing 787 ya Shirika la United iliyokuwa ikiruka kutoka London kwenda Houston ililazimika kugeuza na kuelekea Newark, New Jersey, juzi sababu ya taa inayoashiria upungufu wa mafuta ya injini kuwaka, ikiwa ni ndege mpya ya pili ya Boeing kutua kwa dharura wiki hii.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga ilisema kwamba ndege namba 125 ya United ilitua salama majira ya Saa 8:10 usiku kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Newark Liberty nje ya Jiji la New York. Mamlaka hiyo imesema itafanya uchunguzi wa tukio hilo.
United lilisema kulikuwa na abiria 218, marubani wanne na wafanyakazi 11 ndani yake, Msemaji wa United, Christine David alisema wengi wa abiria hao walihamishiwa kwenye Boeing 767, ambayo iliondoka Newark na kutarajiwa kuwasili mjini Houston juzi jioni.
Msemaji wa Boeing Kate Bergman alisema kampuni hiyo itashughulika na kampuni ya iliyotengeneza injini ya General Electric Co., kufanya matengenezo na kazi ya kujaribu na kuirejesha ndege hiyo kuendelea na kazi angani.
Bergman alisema kwamba tukio hilo halikuhusishwa na jingine la kutua kwa dharura lililohusisha ndege ya United Boeing 787 mapema wiki hii.
Jumanne ndege ya United iliyokuwa ikielekea Tokyo kutoka Denver ilibadili uelekeo na kwenda Seattle sababu ya kile shirika hilo la ndege ilichoeleza kama suala la kichuja mafuta. Shirika hilo la ndege liliwaweka takribani abiria 200 kwenye hoteli moja usiku mzima, kisha kuwasafieisha kwenda Tokyo Jumatano kwenye ndege nyingine ya 787.
Ndege aina ya 787, ambayo Boeing huiita Dreamliner, iko chini ya uchunguzi makini usio wa kawaida sababu zilisitishwa duniani kote kwa miezi mitatu baada ya betri zake kupata joto mno kwenye ndege zake mbili.
Boeing imeunda upya mfumo wa betri kukidhi viwango vya FAA, na ndege duniani kote ilianza tena kutumia ndege hizo mwezi uliopita. United ni shirika pekee la ndege kutumia ndege hizo 787.
"787 ni ndege bora, na tunafahamu itaendelea kupokea umakini mkubwa pale matukio ya uwajibikaji yanapotokea katika huduma," alisema Bergman, msemaji wa Boeing.
Dreamliner ni ndege za Boeing zilizotumia teknolojia ya hali ya juu kabisa, zikiwa zimeundwa kwa kutumia malighafi zenye uzito mwepesi na ubunifu mwingine kuwezesha kutumia mafuta kidogo.
Ulaji wake huo mdogo wa mafuta unaifanya kufaa zaidi kwa safari ndefu zikiwamo safari za kimataifa.