JERAHA USONI KWA MTOTO LAIKOSESHA FAMILIA SAFARI YA NDEGE...

Jeraha usoni kwa mtoto huyo, Robyn lililoiponza familia hiyo kwenye ndege.
Familia moja imetupwa nje ya ndege waliyokuwa wasafirie kwenda kwao baada ya likizo sababu ya mpasuko kidogo kwenye uso wa binti yao ulikuwa kinyume cha tahadhari za kiafya na usalama.

Robyn, mwenye miezi 19, alikuwa amejigonga shavu lake kwenye rejeta mwishoni mwa mapumziko yao ya siku nne mjini Jersey.
Lakini pale wazazi wake laura, mwenye miaka 36, na John Maitland, mwenye miaka 33, walipojaribu kupanda ndege yao ya easyJet kwenda Newcastle, mfanyakazi wa ndege hiyo akagundua jeraha hilo chini ya jicho la kushoto la Robyn.
Alimtaarifu rubani huyo na familia hiyo ikaelezwa wanatakiwa kushuka kwenye ndege hiyo.
Waliachwa wakiwa hawajui la kufanya mjini Jersey hadi walipoweza kupata cheti cha matibabu kuonesha Robyn alikuwa salama kuweza kusafiri.
Na katika kukuza suala hilo, walidai walilazimika kulipia Pauni za Uingereza 600 kupata malazi mbadala wakati wakisubiria jeraha hilo liponywe.
Laura, anayetokea Morpeth, Northumberland, alisema familia hiyo haikufikiria mpasuko huo mdogo ulikuwa jambo kubwa hivyo waliendelea kuelekea Uwanja wa Ndege na walishitushwa na uamuzi wa mfanyakazi wa kwenye ndege.
Alisema: "Sikuweza kuamini. Nilianza kulia na nilikuwa nikimwomba, nikisema "hii ni dhihaka, tunakwenda tu Newcastle, ni takribani safari ya saa moja", lakini alisisitiza kwamba asingeweza kutusafirisha.
"Rubani huyo alisema kwamba jicho ni eneo nyeti - asingeweza kusema kama litakuwa katika hali ya hatari wakati ndege ikiwa angani.
'Alitakiwa kufikiria kuhusu usalama wa abiria wengine wote'. Niliendelea kusema sio jicho lake, ni ngozi chini ya jicho lake.
"Ni alama ndogo tu nyekundu usoni mwake. Haikuwa imechimbika kwa ndani. Halikuwa likichuruzika damu kabisa.
"Alisema asingeweza kusema kitakachotokea, kama angeweza kulipuka au kitu kama hicho.
"Vitu vyetu vyote vilishushwa kwenye ndege. Kama tungekaidi kuondoka wangeita polisi kutusindikiza. Ndege nzima walikuwa wakitutazama. Hakika ilikuwa inaaibisha."
easyJet inasema uamuzi huo ulichukuliwa kwa manufaa ya mtoto huku jeraha lake likiweza kuwa katika hali mbaya wakati wa safari.
Familia hiyo ilitakiwa kukata tena tiketi pale watakapokuwa wamepata cheti cha matibabu kinachosema Robyn alikuwa salama kusafiri.
Laura alisema: "Daktari huyo alisema alifikiri ilikuwa dhihaka. Alisema 'unatania'.
Hatahivyo, ndege nyingine ya kwenda Newcastle ilikuwa siku tatu baadaye na familia hiyo inasema hawakupatiwa msaada wowote kupatiwa makazi au usafiri.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item