TONY BLAIR AAMBULIA URITHI WA PAUNI 80,000 KWA BABA YAKE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/06/tony-blair-aambulia-urithi-wa-pauni.html
Hazina ya Tony Blair ya mamilioni ya pauni imepokea nyongeza ya Pauni 80,000 kutoka kwenye wosia wa baba yake, Leo.
Kumbukumbu wa uthibitisho wa wasia zimebainisha kwamba Leo, mzee wa zamani wa mahakama na mwalimu wa sheria ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 89 Novemba mwaka jana, aliacha mali zenye thamani ya Pauni 295,000.
Wasia wake, ulioandikwa mwaka 2005, uliacha urithi wa Pauni 50,000 kwa binti yake Sarah, mwenye miaka 56, ambaye hajaolewa. Mali iliyobaki kisha ikagawanywa kati ya watoto wake wote watatu, ikimaanisha Sarah, Blair na kaka yao mkubwa Sir William, mwenye miaka 63, Jaji wa Mahakama Kuu, kila mmoja akipokea Pauni 80,000.
Blair, mwenye miaka 60, alikuwa karibu sana na baba yake na alimrithisha mtoto wake wa mwisho jina la baba yake.
Waziri Mkuu huyo wa zamani ana sifa mbaya ya usiri kuhusu utajiri wake, huku sehemu kubwa ya mapato yake tangu aondoke madarakani mwaka 2007 ikiwa imefichwa katika mitandao ya makampuni binafsi.
Blair anaingiza mamilioni ya pauni kwa mwaka kutoka katika biashara zake za ushauri na serikali. Pia ni mmoja wa wazungumzaji wanaolipwa zaidi duniani kwenye mikutano.
Ilibainishwa mwezi uliopita jinsi Tony Blair na mkewe, Cherie walivyoongeza nyumba namba nane kwenye orodha inapanuka ya mali zao.
Kama ununuzi wa nyumba yao ya saba, ukigharimu Pauni milioni 1.35 mwezi Septemba, fedha taslimu zililipwa tena pale waliponunua upesi nyumba ya Pauni 600,000 kwa ajili ya dada mdogo wa waziri mkuu huyo, Sarah Blair.
Nyumba hiyo - iliyoko takribani maili moja kutoka lilipo hekalu la Blair la Buckinghamshire ambalo liliwagharimu Pauni milioni 5.75 mwaka 2008 - lilinunuliwa Siku ya Wapendanao mapema mwaka huu.
Nyaraka za Msajili wa Ardhi zinaonesha linamilikiwa kwa pamoja na 'sawasawa' na Sarah na Cherie Blair.
Nyumba hizo ambazo Blair amenunua kwa ajili ya watoto wao pia zinamilikiwa kwa pamoja na mke wa Blair.
Blair, anasemekana amekuwa akimlinda dada yake, ambaye hajaolewa, hana watoto na kutoonekana hadharani.
Amewahi kusema wao na kaka yao Bill walikuwa karibu mno na kwamba mara kwa mara alikwenda kwa ndugu zake kwa ajili ya msaada wa kiroho.
Hadi hivi karibuni Sarah alikuwa akiishi kwenye ghorofa lenye thamani ya Pauni 450,000 huko Islington, North London.
Akina Blair pia waliishi Islington hadi wakati wa uchaguzi wa mwaka 2007 pale walipohamia Namba 10 na kuuza nyumba yao huku wakishuhudia ikipaa kwa thamani.
Sasa makadirio ya jumla ya thamani ya nyumba zao nane katika kijitabu chao zinakaribia Pauni milioni 21.
Blair anasifika kujipatia Pauni milioni 20 kwa mwaka kutokana na kazi za kuishauri serikali, hotuba na kazi za ushauri na ameimarisha hazina hiyo hasi kufikia Pauni milioni 60.
