SABABU ZA KIFO CHA WHITNEY ZAANIKWA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/03/sababu-za-kifo-cha-whitney-zaanikwa.html
Sababu za kifo cha Whitney Houston zimethibitika rasmi kwamba muda mfupi baada ya kufariki zilionekana dawa za kulevya aina ya cocaine kwenye mfumo wake wa damu, imefahamika.
Hii ni kwa mujibu wa kampuni la Los Angeles County Coroner iliyobeba, kuchunguza na kuandaa mwili wa mwanamuziki huyo kwa ajili ya zoezi zima la mazishi.
Hivi punde, kampuni hiyo imetoa ripoti rasmi ya sababu za kifo cha Whitney ikisisitiza kuwa maradhi ya moyo na matumizi ya cocaine yaliharakisha kifo cha mwanamuziki huyo.
Maofisa wa kampuni hiyo wameendelea kusema uchunguzi huo umebaini pia chembechembe za mihadarati (marijuana), dawa za kulainisha misuli (aina ya Flexeril) na dawa za aleji (aina ya Benadryl) kwenye mfumo wake wa damu.
Chanzo cha habari hizi kilicho jirani na timu ya wachunguzi kimesema kwamba “inawezekana kabisa” Whitney alikuwa na maradhi ya moyo yaliyosababisha kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu hatimaye kufariki dunia.
Maradhi ya moyo yanaweza kuibuka baada ya kuzidiwa nguvu kwa mishipa ya damu (arteries) kunakosababishwa na matumizi ya cocaine.
Awali iliripotiwa kuwa Whitney amekutwa amekufa bafuni kwenye Hoteli ya Beverly Hilton mwezi uliopita na vidonge kadhaa vikiwemo Xanax, Ibuprofen na Midol vimekutwa chumbani kwake.
Lakini wachunguzi hawakukuta ushahidi wowote wa cocaine ndani ya chumba cha hoteli hiyo.
Vyanzo vya kisheria vimeeleza kuwa tangu mwanzo hawakumshuku mtu yeyote na wala tukio hilo halihusiani ya jaribio la kujiua.
Hata hivyo, familia ya Whitney ina mashaka kuwa kifo chake kimetokana na hujuma.
WAKATI HUOHUO Aliyewahi kuwa rafiki wa kiume wa Whitney, Ray J ameibuka hadharani na kukanusha vikali tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba yeye ndiye chanzo cha kifo cha mwanamuziki huyo.
Taarifa zilizozagaa zimemtuhumu Ray J kuwa ndiye aliyekuwa akimuwezesha na kumpelekea dawa za kulevya Whitney ambazo zimeelezwa ndizo zilizopelekea kifo chake.
Ray J ameeleza kusikitishwa na shutuma zilizoelekezwa kwake na dada wa Bobby Brown, Leolah kwenye televisheni akisema kwamba Ray J ndiye wa kulaumiwa kwa kifo cha Whitney. Ameziita tuhuma hizo kuwa ni upuuzi.
Lakini vyanzo vya habari vimeeleza kwamba siku ya kifo cha Whitney, Ray J hakuwapo kabisa maeneo ya jirani na tukio. Alikuwa San Diego.