BOBBI KRISTINA AFUTIWA KESI YA KUINGIA CASINO...

Imefahamika kwamba Bobbi Kristina hatoshitakiwa kwa kuingia na kucheza kamari kwenye casino ya Vegas mwezi uliopita.
Polisi wamefuta kesi hiyo kutokana na kukosekana ushahidi wa kutosha kwamba Bobbi, ambaye ni binti wa mwimbaji nyota wa zamani, Whitney Houston, alivunja sheria kwa kuingia humo akiwa na umri mdogo usioruhusiwa.
Video kadhaa zilimuonesha Bobbi Kristina ambaye ana miaka 19 akicheza kamari katika moja ya mashine huku akiwa ameongozana na rafiki yake wa kiume, Nick Gordon mwenye miaka 22 kwenye casino ya MGM Grand. Umri ulioruhusiwa kisheria kuingia casino mjini Las Vegas ni kuanzia miaka 21.
Kama ilivyoripotiwa, tukio hilo lilikuwa likichunguzwa na mamlaka zinazohusika za Bodi ya Kudhibiti Kamari ya mjini Nevada, lakini Naibu Mkuu wa Bodi hiyo, David Salas alisema, "Tumemaliza uchunguzi wetu na hakuna ushahidi wa kutosha katika madai ya uvunjaji sheria."
Salas aliongeza, "Tunafuta kesi."
Ilielezwa kuwa MGM walitoa ushirikiano mkubwa kwa Bodi hiyo wakati wote wa kuchunguza madai hayo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item