MICHAEL JACKSON ATAKIWA KULIPA FIDIA DOLA BILIONI MOJA...

Mfalme wa miondoko ya Pop, Hayati Michael Jackson 'Wacko Jacko' ameingia kwenye mzozo kwa kufunguliwa mashitaka ya fidia ya Dola za Marekani bilioni moja kufuatia madai ya kutoa taarifa binafsi kuhusu maisha ya mwanamke mmoja kwenye miziki yake, hii ni kwa mujibu wa hati ya mashitaka ambayo vyanzo vya habari vimethubutu kuiita 'ya kipuuzi.'
Kimberly Griggs amefungua kesi mjini San Diego akidai kuwa yeye na Michael Jackson walikuwa na mahusiano yaliyoanza mwaka 1979, ambayo alisema yalihusu albamu zake za "Off the Wall," "Thriller," "Bad," "Dangerous," pamoja na ile iliyotikisa duniani ya "Number Ones."
Griggs ambaye ametumikia miaka kadhaa jela kwa kosa la uporaji na utekaji, anadai aliombwa Michael Jackson kusambaza siri zake binafsi katika nyimbo zake, kwa makubaliano mambo yakienda mazuri atampatia hatimiliki ya nyimbo hizo.
Alisema alishangazwa pale Michael Jackson alipofariki na yeye kuondolewa kabisa kwenye himaya yake.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliandikwa kwa mkono, Griggs anataka alipwe fidia ya Dola za Marekani bilioni moja.
Hakukuwa na majibu yeyote ya simu kutoka kwa watu wa karibu wa Michael Jackson kujibu tuhuma hizo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item