WAWEKA REKODI MPYA MICHUANO YA EURO 2012...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/waweka-rekodi-mpya-michuano-ya-euro-2012.html
PRZEMYSLAW TYTON ambaye ni Kipa namba mbili wa Poland, ameweka rekodi ya kuwa kipa wa kwanza kuokoa penalti ya nahodha wa Ugiriki, Giorgos Karagounis katika michuano ya Euro 2012.
GIORGOS KARAGOUNIS ambaye ni nahodha wa Ugiriki, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kukosa penalti katika michuano ua Euro 2012 baada ya kupiga penalti iliyoishia mikononi mwa kipa wa Poland, Tyton.
ALAN DZAGOEV amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao mawili katika mechi moja kwenye michuano ya Euro 2012. Alifunga mabao hayo dhidi ya Czech katika mechi ambayo Urusi iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 iliyochezwa kwenye Uwanja wa Stadion Miejski mjini Wroclaw.
CARLOS VELASCO CARBALLO ameendeleza rekodi yake ya mwamuzi anayesifika kwa kumwaga kadi nyekundu katika mechi anazochezesha ambapo katika mechi yake ya kwanza tu ya Euro 2012 tayari ametoa kadi mbili. Kumbukumbu zinaonesha mwamuzi huyo wa Hispania ametoa kadi nyekundu 16 katika mechi 19 za Ligi Kuu ya Hispania alizochezesha msimu ulioisha.
***Kama ulikuwa hujui, Poland na Ugiriki inaweza ikashika nafasi za juu kama moja ya mechi iliyokutanisha wachezaji wenye majina magumu zaidi na kuwapa shida watangazaji. Unahitajika umakini wa hali ya juu kutamka majina haya, la sivyo... ROBERT LEWANDOWSKI wa Poland ameweka rekodi ya kuwa mfungaji wa bao la kwanza katika michuano ya Euro 2012 akifunga dhidi ya Ugiriki katika dakika ya 17 ya mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 na kuhudhuriwa na mashabiki 56, 826 kwenye Uwanja wa Stadion Narodowy mjini Warsaw.