RODNEY KING AFARIKI DUNIA AKINYWA NA KUVUTA BANGI...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/rodney-king-afariki-dunia-akinywa-na.html
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mchumba wa Rodney, Cynthia Kelley amewaeleza marafiki Rodney alikuwa akivuta mihadarati wakati fulani, kabla ya kwenda kulala saa 8:00 usiku.
Imeelezwa Cynthia amesema baadaye alimuona Rodney majira ya saa 11:00 alfajiri pale alipoamshwa naye. Vyanzo vimesema Cynthia alimkuta Rodney akiwa uchi, akijigonga kwenye glasi, na ndipo akamuuliza, "Kuna tatizo gani, Rodney?"
Cynthia amewaeleza marafiki kisha alienda kunyakua simu yake pale aliposikia kishondo kikubwa. Kisha alienda nyuma na kumkuta akiwa amezama kwenye bwawa na kuita polisi.
Madaktari wa huduma ya kwanza walijaribu kuokoa maisha ya Rodney lakini ikashindikana.