TBL YASAIDIA MRADI WA MAJI CHUO CHA MT. AUGUSTINE...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/tbl-yasaidia-mradi-wa-maji-chuo-cha-mt.html
Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Stephen Kilindo (katikati) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 53, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha St. Augustine (SAUT), Padri Thadeus Mkamwa (kulia) katika hafla iliyofanyika chuoni hapo juzi. Anayeshuhudia kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho Utawala na Fedha, Padri Peter Mwanjonde. Msaada huo ni kwa ajili ya mradi wa maji chuoni hapo pamoja na kilimo cha umwagiliaji.