ANAYEITWA 'MWANAMKE ANAYETISHA ZAIDI DUNIANI' ATUNGA KITABU KINGINE...

KUSHOTO: Lizzie alipokuwa mtoto. JUU: Lizzie akiwa mezani na virutubisho mwili tele. CHINI: Lizzie (katikati) akiwa na familia yake. KULIA: Lizzie alivyo sasa.
Alidhihakiwa na kukodolewa macho mitaani na kuitwa 'mwanamke anayetisha zaidi duniani' na wanyanyapaaji wasiojali.
Lakini, baada ya miaka ya mateso na kujihofia, Lizzie Velasquez amesema hatimaye amedharau kashfa zote kuhusu muonekano wake na kuzichukulia kama 'maneno tu'.
Lizzie anayetokea austin, mjini Texas, alizaliwa bila mkusanyiko wa seli za shahamu mwilini - ikimaanisha hakuwa na mafuta mwilini na, licha ya kula milo 60 midogo midogo kwa siku, akaishia kuwa na uzito wa kilo 58 tu.
Hali hiyo inayotokea kwa nadra bado inaumiza vichwa madaktari na inafikiriwa kuathiri wawili tu kati ya watu wote duniani.
Lizzie sasa ameandika kitabu cha pili kuhusu mapambano yake kuweza kukubalika na matumaini kuwa itasaidia wengine wanaopitia hali kama yake.
Katika kitabu hicho alichokiita 'Be Beautiful, Be You' (Yaani Kuwa Mrembo, Kuwa Halisia), mwanamke huyo mwenye miaka 23 mwanafunzi wa chuo ameshauri hatua za kuwa wa kipekee, jinsi ya kupata na kutunza marafiki wazuri na jinsi ya kukabiliana na wanyanyapaaji na mitazamo hasi.
Alizungumza na kipindi cha Dr. Drew Pinsky Jumanne usiku kuhusu uzoefu wake, Lizzie alisema wakati wanyanyapaaji walipoanza kumshambulia kupitia mtandao wa intaneti ilikuwa ngumu sana.
Alimweleza Dr. Drew: "Mimi ni binadamu... ni dhahiri hivi vitu vitakuumiza... (lakini) Lakini sitaacha hivi vitu vinianike."
Hatahivyo Lizzie amebaini watu wanaosambaza maoni hayo ya kashfa kwenye mtandao kuwa ni wapuuzi tu wanaojificha nyuma ya skrini za kompyuta zao.
"Mwisho wa siku, haya yanabaki kuwa ni maneno tu," Lizzie alimweleza Dr. Drew. "Kama wana fahari sana, basi wanatakiwa kujitokeza sura zao."
Alipoulizwa jinsi anavyokabiliana na kukodolewa macho mitaani, Lizzie alisema: "Naanza kutaka kuwafuata hawa watu na kujitambulisha au kuwapa kadi yangu na kusema, "Habari, Mimi ni Lizzie - pengine utaacha kunikodolea macho na kuanza kujifunza"."
Lizzie pia alibainisha kwamba hana shauku yoyote kufanana na warembo nyota.
Alisema: "Najihisi nina furaha mno sifanani na mastaa wa huko nje ambao ni warembo, sababu kuna mambo mengi yaliyoambatana na hayo.
"Watu wanafikiri "ni mrembo sana, lazima atapigwa bumbuwazi". Kwakuwa sifanani na hivyo kwamba ni bora sababu watu watanifahamu uhalisia wangu."
Lizzie alizaliwa wiki nne kabla ya muda wake akiwa na uzito wa kilo 2.10. Madaktari waligundua kulikuwa na kimiminika cha kutosha kilichokuwa kimemkinga katika mji wa mimba.
"Walitueleza hawakujua aliwezezaje kuishi," mama wa Lizzie, Rita mwenye miaka 42 ambaye ni Katibu wa Kanisa alisema.
"Tulilazimika kununua nguo za wanasesere kwenye maduka sababu nguo za watoto wadogo zilikuwa kubwa sana kwake." Madaktari hawakuweza kumpima hivyo waliwaandaa wazazi wa Lizzie kupokea taarifa mbaya wakati wowote.
"Walitueleza kamwe asingeweza kutembea, kuongea au kuishi maisha ya kawaida," alisema mama yake, ambaye ana watoto wengine wawili aliozaa na baba wa Lizzie, Lupe - watoto wote hao wakiwa walingana rika na kimo.
Licha ya ubashiri huo ubongo wa Lizzie, mifupa na viungo vya ndani viliendelea kukua kama kawaida lakini siku zote aliendelea kuwa mdogo sana.
Akiwa na umri wa miaka miwili alikuwa na uzito wa kilo 15 tu - sawa na uzito anatakiwa kuwanao mtoto wa miezi mitano.
Kitabu chake kipya kimeingia mtaani juzi, Septemba 13.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item