BABU WA MIAKA 90 ASHITAKI WAZAZI WA MKEWE WA MIAKA 15...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/babu-wa-miaka-90-ashitaki-wazazi-wa.html
Kikongwe wa miaka 90 raia wa Saudi Arabia ameishitaki familia ya binti aliyemuoa mwenye miaka 15 baada ya kujifungia mwenyewe ndani ya chumba katika usiku wa siku yao ya harusi.
Mtoto huyo aliyejawa hofu alijifungia mlango kwa ndani hivyo kumfanya mumewe mpya ashindwe kuingia ndani katika siku yao ya kwanza tangu waoane, na siku mbili baadaye alitoroka na kurejea nyumbani kwa wazazi wake.
Sasa mumewe huyo ambaye ni mtu mzima anataka arejeshewe pesa zake huku akidai kuwa aliwalipa wazazi hao Pauni za Uingereza 10,767 (zaidi ya Shilingi za Kitanzania milioni 27.6) kwa ajili ya mtoto huyo hivyo kuweza kumuoa.
Kikongwe huyo mwenye miaka 90 alisema alilipia mapambo ya bibi harusi kwa mama wa msichana huyo mdogo mwenye asili ya Saudi Arabia na baba mwenye asili ya Yemen, kufanya ndoa hiyo 'kisheria na sahihi', gazeti la Al Arabiya liliripoti.
Mipango ya ndoa ya binti huyo mwenye miaka 15 imetema cheche za ukatili na kushutumiwa vikali katika Saudi Arabia ambapo wanaharakati kupitia mtandao wa Twitter wameuita ni biashara ya kusafirisha watoto na ukahaba.
Mwanachama wa Umoja wa Kitaifa wa Haki za Binadamu Saudi Arabia (NSHR), Suhaila Zein el-Abedin amezitaka mamlaka 'kumwokoa mtoto huyu kutoka katika janga,' akiongeza kwamba ndoa katika Uislamu lazima iwe kwa ridhaa ya mhusika.
Pia alilaumu wazazi wa binti huyo kwa kukubali zawadi za bibi harusi na kumuozesha binti yao kwa mwanaume aliyemzidi miaka 75, akisisitiza umuhimu wa kuweka umri wa chini wa kuolewa uwe miaka 18 katika Saudi Arabia.