DEREVA TEKSI ALIYEMUUA MWENDESHA BAISKELI ATOZWA FAINI SH. 91,000!...

KUSHOTO: Dereva teksi, Ichhapal Bhamra. KULIA: Mwendesha baiskeli, Tom Ridgway.
Dereva taksi aliyemuua mwendesha baiskeli mwenye miaka 20 baada ya kumgonga kwa gari lake na kumgongesha kwenye mti ameachiwa mahakamani baada ya kulipa faini ya Pauni za Uingereza 35 (karibu Shilingi 91,000 za Kitanzania).
Familia ya mwanafunzi huyo, Tom Ridgway imeshutumu vikali faini hiyo 'ya matusi', ikisisitiza adhabu hiyo haitoi haki kwa 'janga kubwa mno' la kifo chake.
Ichhapal Bhamra mwenye miaka 54, aliubeba mwili wa kijana huyo kwenye boneti la gari lake kwa mita 90 baada ya kumgonga kwenye mtaa katika moja ya vitongoji vya mjini Birmingham.
Lakini shitaka pekee alilokabiliwa nalo lilikuwa kuendesha bila uangalifu na kuchukua tahadhari, likimwacha na alama tatu katika leseni yake baada ya kupatikana na hatia kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Solihull.
Mahakama ilielezwa kwamba Tom alikuwa akiendesha baiskeli kutoka nyumbani kwake huko Hall Green katika Solihull Juni 27 ndipo alipogongwa na taksi ya Bhamra.
Mwendesha mashitaka Malcolm Stoddat alielezea jinsi mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Bournemouth alivyoning'inia kwenye boneti la Toyota Previa - na kusababisha shangazi wa muathirika kumwaga machozi wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo.
Dereva huyo alivurumisha gari barabarani kwa mita 90 baada ya kugongana, kubamiza alama za barabarani na mwishowe kujikita kwenye mti.
Tom alikimbizwa hospitali, ambako alifariki dunia muda mfupi baadaye.
Upande wa mashitaka haukuweza kukadiria sababu ya ajali hiyo, na haukuweza kuthibitisha kama kifo cha mwendesha baiskeli huyo kilisababishwa na ajali ya kwanza au baada ya safari hiyo ya mita 90 akiwa kwenye boneti la teksi.
Bhamra baada ya hapo alishitakiwa tu kwa kuendesha bila uangalifu na tahadhari, ingawa aliisalimisha leseni yake ya teksi kwa hiari, uamuzi uliopokelewa na familia ya Tom.
Mama wa mwanafunzi huyo, Liz alisema faini hiyo ilikuwa 'matusi', akaongeza: "Inatisha. Hakuna kiwango kinachoweza kufidia uhai wake.
Wakili wa utetezi Ian Bridge alisema Bhamra, dereva teksi kwa miaka 26, anasumbuliwa na shinikizo la tangu ajali hiyo na kujihisi hawezi kuendesha.
"Tangu ajali hii, hakuna siku inayoweza kupita bila kuwa na mawazo kuhusu machungu inayopata familia ya Tom, yaliyosababishwa na kumpoteza kijana wao," alisema.
"Anatamani kama angerudisha nyuma mshale wa saa."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item