TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAKATAA UTEUZI WA RAIS...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/tume-ya-taifa-ya-uchaguzi-yakataa.html
Jaji mstaafu Damian Lubuva. |
Katika kuhakikisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inakuwa huru na hivyo kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima, uongozi wa Tume hiyo umewasilisha kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba maoni kadhaa, ikiwa ni pamoja na kumtaka Rais asifanye uteuzi wa moja kwa moja wa viongozi wa tume.
Badala yake, imeshauriwa mchakato wa uteuzi wa wajumbe wake kuanzia kwa kamati ya wataalamu, jopo maalumu la Watanzania wanaokubalika katika jamii, wathibitishwe bungeni na ndipo Rais afanye uteuzi.
Aidha, baada ya uteuzi, wajumbe waapishwe na Jaji Mkuu wa Tanzania, badala ya Rais. Wameshauri pia kubadilishwa jina la Tume, kuwepo kwa mahakama ya masuala ya uchaguzi, mbunge aruhusiwe kuhama chama na `kofia’ ya ubunge na pia kuwe na mgombea binafsi.
Mapendekezo hayo yaliwasilishwa jana mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva.
Akiwasilisha, alisema ni vema Katiba mpya ikaanzisha utaratibu wa uwazi zaidi wa uteuzi utakaowajumuisha wadau wa Uchaguzi kwa njia moja au nyingine, ikihusisha wataalamu wa masuala ya uchaguzi, Sheria na jamii kisha mapendekezo yapelekwe bungeni kabla ya kuwasilishwa kwa Rais kwa uteuzi rasmi.
Kwamba, kama vyombo hivyo vitatu katika hatua tofauti vitapendekeza majina ya wajumbe wa Tume na baadaye kuwasilishwa kwa Rais ili aweze kuteua Mwenyekiti na makamu Mwenyekiti miongoni mwao, itaondoa dhana ya wajumbe hao kuwa na utii kwa Rais.
“Kwa kuwa Bunge ni chombo ambacho kinawakilisha wananchi kwenye majimbo na kata mbalimbali ni vema ukawekwa utaratibu utakaowezesha wajumbe wake kuthibitishwa na Bunge Kabla ya kuteuliwa na Rais,”alisisitiza
Kutokana na hali hiyo na mengineyo tume inapendekeza kuanzishwa kwa Tume huru ya Uchaguzi itakayojulikana kama Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kutoa sura kuwa uhuru wa Tume unaanzia tangu kwenye jina la Tume.
Alisema Katiba ndio sheria mama hivyo mambo yote ya msingi ya nchi huanzia kwenye katiba, hivyo kubadilishwa jina na kuweka neno ‘huru’ kunaweza kubadili fikra za wadau juu ya Tume ya Uchaguzi.
Lubuva alisema NEC imependekeza kuwa sheria itoe mwanya kwa uamuzi wake kuhojiwa Mahakamani, badala ya kusubiri mpaka wakati wa kuwasilisha kesi ya Uchaguzi.
Hivyo imependekeza katika katiba mpya ipanue wigo wa Demokrasia kwa kuanzisha Mahakama ya mambo ya Uchaguzi ili kuwezesha wadau au wananchi ambao hawakubaliani na Uamuzi wa tume kupata nafasi ya kukata Rufaa.
“Pia Mahakama hii itaifanya Tume Huru ya Uchaguzi isionekane kuwa juu ya sheria na kuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa uadilifu na umakini zaidi,na mahakama hii iwe ya muda maalumu inapohitajika tu huku muda wa kutekeleza majukumu yake uwe wa haraka,” alisisitiza
Jaji alisema licha ya Tume kupendekeza kuendelea na utaratibu wa uchaguzi ndogo, bado kuna umuhimu wa Katiba mpya kutoa utaratibu wa kudhibiti vyama vya siasa na wanasiasa kuhama na kufukuzana ndani ya vyama bila kuathiri nafasi ya uwakilishi ya kiongozi husika.
“Iwapo Mwakilishi atafukuzwa na kuhamia chama kingine basi ahame na kiti chake cha uwakilishi kama Ubunge, Udiwani au uenyekiti wa kijiji, Kitongoji au Mtaa,“ alisema.
Alisisitiza kuwa ili mbunge aweze kuhama na kiti cha uwakilishi, haki ya Mgombea binafsi hapana budi kuangaliwa kwenye katiba mpya,jambo litakalosaidia kupunguza wingi wa chaguzi ndogo zisizo za lazima.
Alisema kwa maana hiyo, uchaguzi mdogo ufanyike mwakilishi wa wananchi anapofariki au kuondolewa mahakamani.
Alisema pendekezo lingine ni kuwa Tume hiyo ipewe mamlaka ya kusimamia chaguzi zote ikiwa ni pamoja na za Mitaa,Vijiji na vitongoji badala ya hali ilivyo sasa chaguzi hizo kusimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu yaani Serikali.
Pia inapendekeza ipewe mamlaka ya kuandaa utaratibu maalum utakaotumika kuwapata wagombea wa nafasi za wanawake wa Viti Maalum katika vyama vyote vya siasa ili kuondoa malalamiko juu ya mfumo wa upatikanaji wa nafasi za wanawake wa viti hivyo.