DK SHEIN AACHIA HURU WAFUNGWA 16 MIAKA 49 YA MAPINDUZI...

Rais Dk Ali Mohammed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, ametoa msamaha kwa wafungwa (Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo) 16 ikiwa ni miongoni mwa sherehe za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964.
Dk Shein ametoa msamaha huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa kisheria chini ya kifungu namba 59 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
 Msamaha huo ambao hutolewa kila mwaka katika kipindi cha sherehe za Mapinduzi huwahusisha wafungwa ambao ni wazee sana, wenye maradhi sugu au wenye vifungo vidogo vidogo na kuonesha nidhamu nzuri chuoni.
Wafungwa  wenye makosa ya wizi wa kutumia nguvu, wizi wa mali ya Serikali, makosa ya kudhalilisha wanawake na watoto, makosa ya dawa za kulevya na wenye makosa mengi ya zamani kwa kawaida huwa hawapewi msamaha.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item