JELA YAMKABILI SAJENTI ALIYEMBAKA BINTI WA MIAKA 12...

KUSHOTO: Sajenti Adrian Rose. KULIA: Eneo walilobambwa wakiwa ndani ya gari mjini Norwich.
Sajenti wa jeshi la polisi ambaye alifanya ngono na msichana wa miaka 12 baada ya kuunda naye urafiki kupitia simu yake ya mkononi anakabiliwa na hukumu ya kifungo jela.
Adrian Rose alifahamiana na binti huyo kupitia mtandao wa BlackBerry Messenger unaotumiwa zaidi na vijana, alijifanya kuwa na miaka 19, na kisha kumpa lifti hadi nyumbani kwa binti huyo Norwich ambako alifanya naye ngono.
Askari huyo mwenye miaka 36, mkazi wa Aldershot huko Hampshire, alijiandaa kukutana na binti huyo na kumwondosha kwenye makazi yao ya askari kwenda kufanya naye mapenzi.
Sajenti huyo wa jeshi alikana mashitaka saba ya ubakaji, sita ya kumteka nyara msichana na kukutana na mtoto kwa madhumuni ya kufanya naye mapenzi.
Mahakama ilielezwa jinsi mahusiano yao yalivyogunduliwa pale polisi walipomwona Adrian akiwa na msichana huyo ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa kwenye bustani huko Norwich, Februari mwaka huu.
Mwendesha mashitaka Clare Matthews aliieleza mahakama kwamba maofisa waligundua suruali za msichana huyo zikiwa hazikufungwa zipu na kulikuwa mipira ya kiume ndani ya gari.
Alipohojiwa, Adrian aliwaeleza polisi: "Ni kama ambavyo ningeweza kufanya chochote na msichana wa miaka 16".
Polisi walimpeleka msichana huyo nyumbani na kugundua mama yake hakuwa kabisa na taarifa kwamba walikutana na Adrian na kwamba alidhani alikuwa na marafiki zake wa rika moja.
Kipimo cha DNA cha Adrian kiligundulika kwenye nguo za msichana huyo.
Clare alisema msichana huyo alikiri mbele ya polisi kwamba alifanya mapenzi na Adrian katika matukio kadhaa ikiwamo hotelini baada ya kukutana naye kupitia mawasiliano ya meseji za BlackBerry.
Alisema alimwambia kwamba alikuwa na miaka 19 na kumlipia vitu kadhaa na kumfanya ajihisi wa kipekee.
Msichana huyo aliongeza kwamba Adrian 'alituliza kabisa sauti'.
Adrian alikanusha kufanya mapenzi na msichana huyo au kujua kwamba alikuwa na miaka 12. Katika taarifa alisema alishitushwa na kukamatwa kwake na kwamba hakufahamu umri wa msichana huyo.
Lakini upande wa mashitaka ulidai kwamba alifahamu fika umri wake halisi na kwamba alikuwa shuleni.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item