HIKI NDICHO KILIMLIZA WAYNE ROONEY MECHI YA KOMBE LA FA...

KUSHOTO: Wayne Rooney akishangilia bao lake. KULIA: Rooney akitokwa machozi kumkumbuka Rosie McLouglin (picha ndogo).
Kilio na kunyoosha mikono juu alikofanya Wayne Rooney baada ya kuifungia Manchester United bao la ushindi katika mechi ya Kombe la FA, ilikuwa ni namna ya kutuma rambirambi kufuatia kifo cha shemeji yake, imebainika.
Baada ya kufunga bao dhidi ya West Ham jioni ya Jumatano iliyopita, alionekana akiwa na hisia kali kwa kubusu  na kuinua mikono yake angani - ikiashiria kumkumbuka Rosie McLouglin ambaye alifariki dunia akiwa na miaka 14, mapema mwezi huu.
Rosie, mdogo wa mkewe, Coleen, alifariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya Rett Syndrome kwa muda mrefu.
Taarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia yake na Rooney ilisema: "Tumehuzunishwa sana, lakini tumebarikiwa kuwa naye kwenye maisha yetu.
"Tutafurahia kumbukumbu nzuri tulizoshiriki naye na upendo aliotuonesha kila mmoja na kila siku."
Rooney, ambaye baadaye alikosa penalti katika mechi hiyo, aliweka tangazo la ukurasa mzima kwenye gazeti moja kutoa rambirambi zake kwa Rosie.
Aliandika: "Malaika wangu Rosie, nitakukumbuka mno. Sitakusahau jinsi ulivyocheka na macho yote makubwa marembo. Wewe ni msukumo kwangu.
"Mungu amekuita, hivyo tunatakiwa tukuache uende, hivyo chukua macho yako na tabasamu lako pana na ifanye pepo kung'ara.
"Siku zote utakuwa na nafasi ya kipekee moyoni mwangu. Nakupenda siku zote na milele. Wako Wayne."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item