MKE WA WAZIRI MWANRI ATOA HADHARANI SIRI ZA MUME WAKE...

Naibu Waziri Aggrey Mwanri.
Kufuatia Naibu Waziri wa  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri kuwa mkali  na kukagua  ujenzi wa  miradi ya kijamii  mkoani Rukwa  kwa umakini  mkubwa  na kubaini mapungufu mengi  mkewe Agnes  Mwanri amefunguka na kusema  ndivyo alivyo  hata akiwa nyumbani  kwao .
Mama Mwanri ambaye  anafuatana  na mumewe katika ziara  ya kikazi  ya siku  sita  mkoani  hapa  ambapo  tayari ameshatembelea   na kukagua  ujenzi wa  maendeleo  katika Halmashauri  za  Kilambo, Sumbawanga na Manispaa ya Sumbawanga  alifunguka na kusema  hayo  juzi  wakati alipokuwa  akiwasalimia  wananchi katika  mkutano  wa hadhara kijiji Wipanga katika Manispaa  ya Sumbawanga .
Alisema;  “msimshangaye mkadhani anajipendekeza   hapana  yeye (Mwanri)  ndiyo alivyo  hata  akiwa  nyumba  nafanya   vitu  vyake  kwa  umakini wa  hali  ya juu  na  hapendi  kudanganywa    wala  kuona  watu  wakidhulumia  haki  zao
“Mume wangu  ndivyo alivyo  hata akiwa  nyumbani  kwanza  hapendi  uonevu  wala udanganyifu wa  aina yeyote ile  yeye siku zote anasimama katika haki… Hivyo  nimeamua kuwaeleza haya   kwa sababu  kutokana na kuwa makini  katika  kazi  zake  hususani anapokagua ujenzi wa miradi,  isieleweke kuwa  anajipendekeza  la hasha yeye  ndivyo  alivyo,” alisema.
Mwanri amekuwa kivutio kikubwa na kumwagia sifa kemkem na  wananchi  katika  maeneo  mbalimbali  alipotembelea na kukagua ujenzi  wa miradi  ya  kijamii  wakidai kwamba  hawajawahi kushuhudia  kiongozi  yeyote wa ngazi  za juu  akikagua ujenzi wa miradi  hiyo  kwa umakini  wa hali  ya juu .
“Sisi  tunasema ameonesha  njia basi  na  viongozi wetu  waige mfano wake uliotukuka  hatujawahi  kushuhudia umakini  wake  Naibu Waziri   huyu  hasa   anapokagua  ujenzi wa miradi ya  kijimii  yaani anafahamu mambo  mengi  ya kiufundi kuliko  hata wahandisi  wenyewe.
“Tunamfananisha na  John Magufuli (Waziri wa Ujenzi)  na Harrison Mwakyembe  (Waziri wa Uchukuzi) kwa hakika hawa watatu  ni  majembe  hatuna  ubishi  nao,” alisena John Ngweshi  kijijini Wipanga .
Lakini licha  ya umakini  wake  pia wengi  wameguswa na uwezo wake wa kuongea katika  mikutano  ya hadhara na ya ndani  kwa  zaidi ya  saa  sita mfululizo  bila kupumzika.
Juzi Naibu Waziri huyo  alikuwa  kivutio  kikubwa   mjini Sumbawanga  pale  alipotembea  kwa miguu kwa  zaidi ya saa moja  akikagua miradi ya ujenzi  wa  barabara  mjini  humo  iliyojengwa kwa  kiwango  cha lami na  Stendi Kuu  ya mabasi.
Kutokana  na umakini wake huo  Mwanri ameweza kubaini  mapungufu mengi ya ujenzi katika  miradi  mbalimbali  ikiwemo  ya  vyumba  vya  madarasa, barabara, majengo  ya  miradi muhimu  ambayo  mengi  yamejengwa  chini  ya kiwango.
Mbali  ya  kuwa makini  hivyo  lakini  pia  anapenda mizaa  kwani  katika siku ya kwanza ya  ziara yake  kijijini Tunko  alibaini  kuwa  jina lake kwenye  mabango ya  matangazo  ya kumkaribisha  katika Halmashauri  ya Sumbawanga  lilikuwa limekosewa  hivyo  alimwagiza  Kaimu Mkuu wa Wilaya  ya Sumbawanga, Moshi Chang’a  kulifuta na kuliandika upya.
“Mimi siwezi kunong’ona  nimesoma kwenye  vitambaa  vya matangazo  ya kunikaribishwa  vilivyotundikwa barabarani  jina langu limekosewa  sasa  kwa sauti  kubwa  nakuuagiza  DC  ulirekebishe mara moja  kabla  sijaondoka hapa,” aliagiza.
Kufuatia agizo  hilo  ililazimu   mawe  yote  ya msingi aliyopangiwa  kuweka  au kuzindua  yalilazimika kurekebisha  herufi  ya mwisho  ya jina lake  la  mwisho.
Lakini pia  alimshukuru  kwa  namna ya pekee  Mbunge wa Jimbo la Kwela  (CCM), Ignas Malocha  kwa kumpatia  heshima ya kipekee  kwa mapokezi aliyomuenzi  ikiwemo kumvalia suti na tai  za gharama kauli  iliyowafanya  wengi  kuangua  kicheko.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item