AKWEPA BILI HOTELINI KWA KISINGIZIO MGONJWA WA MOYO, AISHIA JELA...

KUSHOTO: Jereny Heath. KULIA: Moja ya migahawa aliyofanya utapeli wake.
Sehemu ndogo muhimu kabisa kwenye chakula cha mgahawa wowote inakuja pale mhudumu anapoleta bili.
Lakini Jeremy Heath alibuni njia mpya kukwepa kulipa - alijifanya kapata shambulio la moyo na kukimbizwa hospitalini.
Kwa takribani miaka mitano alikuwa mteja ambaye mameneja wa mgahawa walitamani asirejee tena kutokana na kuwatapeli mamia ya pauni katika bili ambazo hazikulipwa.
Aliweza kuagiza vinywaji na chakula kabla ya kujifanya anaumwa pale anapokuwa amemaliza chakula kwenye sahani yake na glasi yake kuwa tupu.
Katika mgahawa mmoja alimweleza mfanyakazi kuwa alikuwa mgonjwa mno na walipiga simu kuomba msaada, lakini alinaswa kwenye kamera za CCTV akimalizia funda lake la pombe wakati akisubiria gari la wagonjwa.
Juzi Heath alikuwa akipata mlo wake wote bure kwa mara nyingine - lakini safari hii akiwa mgeni wa Magereza. Heath, mkazi wa Preston, ambaye anatumia kiti chenye magurudumu na kusumbuliwa na uti wa mgongo, alikuwa akianza kutumikia kifungo cha wiki sita jela baada ya kukiri udanganyifu kwa muonekano wa uongo.
Hakimu huko Blackpool alielezwa kwamba alikuwa 'mlaji na mtorokaji' ambaye amekuwa kero kwa wamiliki wa migahawa katika nchi tatu.
Alisemekana kuwa alianza tabia yake ya udanganyifu mwaka 2008 baada ya kuporomoka vibaya kwa afya yake na alisafiri ukanda wote wa Kaskazini mwa Uingereza akifurahia karamu baada ya karamu.
Alialikwa kwenye migahawa na baa huko Cumbria, Lancashire na Greater Manchester ambako aliagiza mlo mzuri na kisha kushushia na glasi kadhaa za bia.
Katika tukio mojawapo alisingizia kwamba kapatwa na matatizo ya moyo na kukimbizwa hospitali na kuishia tu kuruhusiwa kutoka baada ya madaktari kugundua kwamba alikuwa mzima kabisa. Wakati mwingine, alisema wazi kwamba hakuwa na pesa za kulipia chakula au kuwaeleza wamiliki wa migahawa kwamba 'mlezi' wake angelipa baadaye.
Alihukumiwa kifungo cha siku sita mwaka jana lakini hamu yake ya kula na kutokomea ilikuwa haizuiliki na aliendelea na mfululizo wa matukio yake ya utapeli mwezi uliopita.
Wakili wake Daniel Harman alisema: "Tatizo halisi la mteja wangu ni pombe - chakula ni kitu kilicho pembeni ya matukio haya. Kitu kimoja cha kukumbukwa ni kwamba hakuweza kutiwa hatiani hadi alipofikisha umri wa miaka 42 ambapo iliambatana na kudhoofika kwa afya yake."
Baada ya kesi hiyo, Paolo Diliberto, meneja wa Thin White Duke mjini Carlisle, alisema: "Mtu huyo alitumia ulemavu wake na kutusomba sisi sote kwa ajili ya safari yake.
"Hafai kabisa na mlolongo huu wa vitu umetusababishia tatizo kubwa hasa katika majira ya sasa ya kiuchumi.
"Alisema alikuwa na maumivu katika moyo lakini hakufahamu kuwa tulimwona kupitia kamera za CCTV akimimina glasi ya bia wakati akingojea gari la wagonjwa.
"Bili haikulipwa sababu tulidhania kwamba alikuwa maskini sana.
"Hatukufikia chochote hadi tulipopigiwa simu na mtu fulani kwenye mtaa wa jirani kwamba amewafanyia kitu kama hiki." Mmoja wa wafanyakazi wa Castle Gardens huko Poulton- le-Fylde, mjini Lancashire, aliongeza: "Alikuja kwenye baa na kusema hakuwa na pesa na kokote pa kwenda.
"Ni wazi alikuwa akitumia ugonjwa wake na tulimwonea huruma.
"Niliishia kuwapigia simu polisi kwa ajili ya ushauri wa kujaribu na kumpatia msaada kidogo."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item