CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/cheka-taratibu_24.html
Mlevi mmoja katangaza baa kwamba ana wasiwasi kuwa yeye ni Mungu! Wenzake walipomuuliza kwanini anafikiria hivyo, mlevi akajibu: "Kila nikifika mtaani kwangu nasikia watu wakisema MUNGU WANGU umelewa tena? Nikifika baa naambiwa MUNGU WANGU umekuja tena? Mkuu wa kituo cha polisi akiniona tu utamsikia MUNGU WANGU hujaacha tu pombe? Nikiendesha baiskeli utasikia MUNGU WANGU atafika kweli?" Walevi wenzake wakasema: "MUNGU WANGU hujielewi tu!" Mlevi akadakia: "Si mnaona eeh!" Kasheshe...