GHOROFA LAPOROMOKA DAR, 60 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/ghorofa-laporomoka-dar-60-wahofiwa.html
Baadhi ya wasamaria na vikosi vya uokoaji wakitoa majeruhi na baadhi ya miili ya watu. |
Kama ilivyo kawaida ya 'wabongo'! Umati wa watu ukikimbilia kwenye eneo la tukio bila tahadhari yoyote. |
Habari zilizotufikia zinasema kwamba watu wapatao 60 wanahofiwa kupoteza maisha baada ya jengo walilokuwa wakiishi kuanguka mapema leo asubuhi jijini Dar es Salaam.
Jengo hilo ambalo liko katika makutano ya Mtaa wa Indira Ghandhi na Morogoro, inaelezwa kwamba lilikuwa bado likiendelea kujengwa huku sehemu ya chini ikiwa imeanza kutumika kwa makazi ya watu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, maiti 14 zimeopolewa kutoka kwenye kifusi cha jengo hilo na zaidi ya majeruhi 30 wamekimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Inaaminika kwamba bado kuna watu walio hai ambao wamefukiwa na vifusi wakiwamo watoto wanafunzi wa madrassa za Kiislamu inayosemekana ilikuwa katika jengo hilo.
Vikosi vya ukoaji vinaendelea na zoezi la uokoaji huku taarifa za hivi punde zinasema kwamba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi naye ameshafika eneo la tukio.
Taarifa zaidi zinasema kwamba kazi ya uokoaji inafanyika katika mazingira magumu kutokana na ukosefu wa vifaa vya kisasa kwa ajili ya kazi hiyo.
Habari zaidi endelea kuperuzi ziro99blog.