ATENGENEZA GARI LA AJABU KWA KUTUMIA MABAKI YA NDEGE...

JUU: Gari hilo likiendelea kuundwa kwenye karakana ya Jeff. CHINI: Gari hilo la ajabu likiwa tayari kwa mashindano. KULIA: Jeff Bloch akiwa ndani ya gari lake hilo la ajabu.
Unaweza tu kuiita Frankenplane.
Jeff Bloch ametengeneza gari ya mashindano ya mabati ya aluminium yenye macho yake juu ya anga - ni sehemu ya ndege ya Cessna 310 ya mwaka 1956 na sehemu ya gari aina ya Toyota minivan la mwaka 1987.
  Imebatizwa jina la ‘Spirit of LeMons’ kwa heshima kuu ya Charles Lindbergh ya ‘Spirit of St Louis,' ndege chotara iliyotumia miezi takribani mitano kutengenezwa.
Gari hilo limekuja kutoka kwenye mfululizo wa mbio za ’24 Hours of LeMons,’ shindano ambalo washiriki wana kikomo cha Dola za Marekani 500 za matumizi kutengeneza gari la mashindano kutokana na vikorokoro.
Bloch, ambaye anafahamika kwenye mbio hizo kama Speedycop, ameunda magari 13 kwa mfululizo huo. Gari lake la Spirit of LeMons, hatahivyo, linaweza kuyapita yote katika mashindano hayo.
Wakati alipoanza, ndege ya Cessna ilikuwa katika hali mbaya, na tayari alishakuwa amenyofoa vipuri vyake vingi.
"Nilikuwa na wanyama wanaoishi ndani yake," alisema.
"Tuliifanyia kazi katika kipindi chote cha baridi - kwenye baridi na kwenye giza na kwenye mvua na theluji."
Lakini kwa malipo ya kazi ya miezi mitano, Bloch alibadili umbo hilo kuwa kitu fulani kinachofanana na risasi ya shaba.
Ndege ya Cessna ilipachikwa kwenye chesisi ya Toyota na kuwa kitu kipya kabisa. Bloch aliweka usukani wa gari na mfumo wa gia.
Lakini muonekano huo ni zaidi katika anga.
Gari hilo jipya linaweza kufikisha mwendokasi wa maili 90 kwa saa na urefu wa futi 27 kutoka kwenye pua yake hadi mkiani.
Bloch alieleza kwamba anapanga kupachika taa za nyuma, taa za mbele, na indiketa ili Cessna hiyo iweze kuchanja mitaani.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item