CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/cheka-taratibu_23.html
Dereva wa bodaboda katika mbio bafuni akipiga kelele eti bafuni kuna mashetani. Wapangaji wenzake kwenye ile nyumba wakatoka kujua kulikoni, ndipo dereva huyo akaanza kuwaeleza huku akihema kwa hofu: "Jamani kila nikijimwagia maji kichwani hayafiki kwenye nywele." Badala ya kumwonea huruma, wapangaji wakaanza kucheka mpaka wanatokwa machozi. Kumbe jamaa alisahau kuvua kofia yake ya kuendeshea bodaboda! Duh...