MZEE MANDELA YU TAABANI, WANANCHI WATAKIWA KUJIANDAA KWA LOLOTE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/mzee-mandela-yu-taabani-wananchi.html
Mzee Nelson Mandela. |
Hali ya Mzee Nelson Mandela ilibadilika na kuwa mbaya sana usiku wa kuamkia leo, kiasi cha kumchochea Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kulitaka taifa hilo kujiandaa kwa taarifa zozote mbaya.
Rais huyo mstaafu mwenye umri wa miaka 94 alishambuliwa na maambukizi kwenye mapafu Jumatano usiku.
Zuma alisema wananchi wa Afrika Kusini wanatakiwa kuwa wakweli kuhusu dalili hizo sababu ya umri wa Mandela.
"Kwa Wazulu, pale mtu anapofariki ambaye ni mzee sana, watu husema amekwenda nyumbani. Nadhani zote hizo ni baadhi ya vitu tunavyotakiwa kuvifikiria," alisema Zuma.
Hii ni mara ya nne katika kipindi cha miaka miwili tu kwa Mandela anayezidi kudhoofika kulazwa hospitalini.
Zuma alisema Mandela alikuwa akiendelea 'vizuri sana' na alisema alikuwa akitarajia kumtembelea hospitalini mapema iwezekanavyo.
Kwa upendo alirejea malenga huyo wa ushairi wa Tuzo za Amani za Nobel kwa jina lake la ukoo, alisema: "Tunawaomba watu wa Afrika Kusini na dunia kwa ujumla kumwombea mpendwa wetu Madiba na familia yake na kuwaweka katika fikra zao.
"Tuna imani kubwa kwa timu ya madaktari na tunajua kwamba watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha anapata anapona."
Chama tawala cha African National Congress kimetaka maombi zaidi kwa Mandela, kama alivyofanya Rais wa Marekani, Barack Obama.
Ofisi ya Zuma ilisema Mandela alikuwa katika hali mbaya na 'anaendelea vema' baada ya matibabu lakini haikuweka bayana wapi hasa alikokuwa akitibiwa.
Msemaji wa ofisi hiyo Mac Maharaj aliongeza baadaye: "Nafikiri tunahitaji kufahamu kwamba madaktari wanamhudumia Madiba kwa umakini wa hali ya juu. Wamechagua kushughulika kwa tahadhari, na wakagundua uwepo wa maambukizi kwenye mapafu, wakadhani kwamba inahitajika kutibiwa haraka sana hasa kwa kuzingatia umri wake na historia yake."
**Timu nzimba ya ziro99blog tunamwombea Mungu amjalie afya njema Mzee Madiba apone haraka na kumjalia afya njema!"