HATARI!! PASIPOTI ZA TANZANIA 'ZAUZWA KAMA NJUGU'...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/hatari-pasipoti-za-tanzania-kama-njugu.html
Idara ya Uhamiaji imeshtukia kuibuka kwa biashara ya ununuzi wa hati za kusafiria za Tanzania, unaofanywa na watu wasio Watanzania.
Wanunuzi hao wanadaiwa kushawishi Watanzania wenye hati hizo, kuziuza kwao kisha watoe taarifa ya kupoteza hati hizo wapatiwe zingine.
Akizungumza na mwandishi katika mahojiano maalumu, Naibu Kamishna wa Uhamiaji anayeshughulikia Huduma, Abbas Irovya alisema kumekuwa na ongezeko la upotevu wa hati hizo kwa watu wanaokwenda miji mbali mbali duniani.
Alisema idara hiyo kwa sasa imeanza kutilia shaka wimbi la upotevu wa hati hizo, kuwa zinauzwa kwa watu wasio Watanzania.
“Idara ina taarifa ya kuwapo wimbi la watu wanaoripoti kupotelewa hati za kusafiria wanapokwenda miji mbalimbali.
“Wasiwasi wetu ni kuwa huenda upotevu huu unatumiwa na raia wasio wema kufanya uhalifu kwa kuziuza kwa watu ambao si Watanzania,” alisema Irovya.
Kwa mujibu wa Irovya, kwa sasa hali ya upotevu wa hati za kusafiria ni kubwa, kwani kwa wastani kila siku hutolewa taarifa za kupotea kwa hati hizo.
Alisema kutokana na hali hiyo, kwa mwaka hati zinazopotea kwa wastani ni 360 na hakuna taarifa za kurejeshwa.
“Ni tofauti na miaka ya nyuma, ambapo kulikuwa na taarifa za kupatikana kwa hati za kusafiria zilizopotea, kwa sasa hilo halipo na wimbi la upotevu linaongezeka.
“Hali hii ndiyo inayotufanya tutilie shaka kuwa huenda hizi hati zinazopotea zinauzwa kwa watu wengine na kuzibadilisha,” alisema.
Irovya alisema ili kupambana na hali hiyo, Idara yake haitampatia hati ya kusafiria mtu aliyepoteza ya awali, mpaka hapo watakapojiridhisha namna upotevu ulivyotokea baada ya kufanya uchunguzi wa kina.
“Tutakuwa makini kuwapa hati ambao wamepoteza za awali, mpaka hapo tutakapofanya uchunguzi wa kina kuangalia mazingira ya upotevu.
“Siku za nyuma tulikuwa tunawatilia shaka na kufuatilia nyendo za mtu anayepoteza mara tatu, lakini sasa tutazidisha udhibiti,” alisema.
Kwa utaratibu wa sasa, mtu aliyepoteza hati ya kusafiria, hutakiwa kutoa taarifa kituo cha Polisi na kutangaza kwenye gazeti na baadaye kupeleka maombi ya kupatiwa hati mpya.
Kwa wale wanaoishi nje ya nchi, hutakiwa kuwa na ripoti ya kupoteza hati kutoka Polisi katika nchi husika, kutangaza kwenye gazeti na kuomba upya.
Irovya aliwataka Watanzania wanaosafiri katika miji mbalimbali duniani, kuwa makini kutunza hati zao na kuacha kuingia tamaa za kuuza kwa watu wengine, kwani kwa hali hiyo watashughulikiwa na mkono wa sheria.
“Tanzania imejijengea heshima kwa mataifa mbalimbali hali ambayo inawavutia wahalifu kuiba na kutumia vibaya hati za kusafiria katika biashara haramu.
“Wananchi wanatakiwa kujua kuwa kuuza au kumhamishia mtu hati yako, ni hatari na utakutwa na mkono wa sheria,” alionya.
Kuhusu kuwapo kwa Watanzania ‘feki’ China, ambao wanaingia nchini humo kwa kutumia hati za kusafiria za Tanzania wakati si Watanzania, Irovya alisema hawana taarifa ya kuwapo Watanzania bandia zaidi ya kusikia kwenye vyombo vya habari.
Alisema pamoja na taarifa hizo kuzisikia kupitia vyombo vya habari, idara hiyo imeshaanza mawasiliano na Ubalozi wa Tanzania nchini China, ili kujua kama kuna tatizo hilo.
Baada ya mawasiliano hayo, alisema hatua zaidi zitachukuliwa na mamlaka husika nchini humo, za kuwasaka watu hao na kuwachukuliwa hatua za kisheria.
Watanzania wanaoishi China, wiki iliyopita walilalamikia kuvamiwa na Watanzania bandia kutoka mataifa mbalimbali, hali inayotishia uhusiano baina ya watu wa nchi hizo mbili.
Katibu wa Jumuiya wa Watanzania waishio China, David Chamla, alitoa kilio hicho mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyepo nchini humo kwa ziara ya kikazi.
"Hawa Watanzania bandia wakishaingia hapa hujitambulisha kuwa ni Watanzania, hata wakiulizwa hati za kusafiria za Tanzania, wanazo, lakini cha ajabu ukiwauliza wanakotoka Tanzania, hubabaika na hata lugha ya Kiswahili hawaijui sawasawa.
“Utakuta mtu anajua kusalimia tu, anasema 'mambo' basi, sasa jamani kuna Mtanzania ambaye hawezi kuzungumza Kiswahili?” Alihoji Chamla.
Wakati huo huo, Irovya amewataka Watanzania kwenda ofisi za Uhamiaji kupata huduma, na kuacha kutumia vishoka na watumishi wasio waaminifu.
“Wananchi waache kutumia vishoka, wafike wenyewe ofisini na watahudumiwa bila kutakiwa gharama za ziada, wasiruhusu kumbukumbu zao zijazwe na watu wengine,” alihadharisha.
Alisema pia idara hiyo ina mpango wa kuja na mfumo wa e-Immigration, ambao watachukua alama za kibaolojia za muombaji wa hati ya kusafiria kwa kompyuta, ili kupunguza tatizo la watu kughushi hati hizo na kufanya uhalifu.
“Hata ukijibadili kwa kufanya upasuaji wa sura, tutakufahamu tu. Dira yetu ni Uhamiaji kwa maendeleo, hivyo tunaruhusu kusafiri kwenda nchi za nje, lakini kwa kufuata utaratibu,” alisema.