MSTAAFU APOKEA KIPIGO KWA KUMKUMBUSHA DEREVA KUWASHA TAA ZA GARI...

KUSHOTO: Mstaafu baada ya kupokea kipigo kikali. JUU: Christopher Graney. CHINI: Samantha Frenton.
Mstaafu ameachwa akiwa hatambuliki kabisa baada ya vijana wawili kumtandika vilivyo wakati alipowapungia kuashiria taa za gari lao zilikuwa haziwaki.

Christopher Graney na Samantha Fenton, wote wana umri wa miaka 19, walimwacha mstaafu huyo mwenye miaka 78 akiwa na mivilio mikubwa ya damu usoni mwake baada ya kumpiga kwenye kituo cha basi.
Wawili hao walishuka kutoka kwenye gari lao, kumsukuma mzee huyo ambaye hakutajwa jina, kisha kumdunda na kumkandika ngumi huku wakimlaza chini akiwa hawezi kujikinga na mashambulizi hayo.
Kisha waliingia kwenye gari lao na kukimbia eneo la tukio, lakini walikamatwa muda mfupi baadaye nyumbani kwao Fenton, huko Bromley, mjini Kent.
Fenton na Graney, wakazi wa Beckenham, wote walitiwa hatiani kwa shambulio la 'kushitusha na kiwendawazimu' lenye lengo la kudhuru mwili kwenye Mahakama ya Croydon.
Muathirka huyo mwenye miaka 78 alimwaga machozi wakati alipoelezwa na polisi kuhusu hatia ya watuhumiwa.
Mnamo Oktoba 15, mwaka jana polisi waliitwa Barabara ya Widmore, huko Bromley, mjini Kent majira ya Saa 6:05 usiku. Walipowasili walikuta mtu mzima akiwa damu imevilia katika uso wake.
Muathirika huyo alikuwa akingojea basi ndipo alipoona gari likipita katika Barabara ya Widmore kwa spidi kali bila kuwa limewasha taa yoyote.
Alipungia mikono kumshitua dereva, lakini ghafla gari hilo lilikasimama mara moja.
Graney na Fenton walikana mashitaka yote, lakini walitiwa hatiani kwa uwiano wa jumla wa 11-1 na baraza la wazee wa mahakama Jumanne iliyopita.
Wawili hao watahukumiwa mnamo Aprili 9, mwaka huu kwenye Mahakama ya Croydon.
Graney pia atahukumiwa kwa shambulio jingine alilotenda mapema Agosti 27, 2011, pale mwanaume mwenye miaka 28 aliposhambuliwa mbele ya kituo cha mafuta cha Total katika Barabara ya Croydon, Beckenham, na akalazimika kupatiwa matibabu ya jeraha kwenye kichwa hospitalini.
Graney amerudishwa rumande akisubiria hukumu yake, wakati Fenton ameachiwa kwa dhamana.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item