HUKUMU YA WAFUASI WA SHEKHE PONDA LEO...

Watuhumiwa wakiwa mahakamani Kisutu, Dar es Salaam.
Hukumu ya kesi ya uchochezi na kufanya maandamano haramu inayowakabili wafuasi 53 wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Issa Ponda inatolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washitakiwa katika kesi hiyo wanadaiwa  kufanya maandamano kwa malengo ya kwenda kumshinikiza Mkurugenzi wa Mashitaka atoe dhamana kwa Shekhe Ponda  na Mukadam.
Hakimu Sundi Fimbo atatoa hukumu hiyo baada ya kupitia majumuisho ya kesi yaliyowasilishwa jana na pande zote mbili kwa njia ya maandishi.
Upande wa Mashitaka ulikuwa na mashahidi tisa na washitakiwa wote waliofikishwa mahakamani hapo Februari 18 mwaka huu walijitetea wenyewe pamoja na mashahidi watatu.
Upande wa Mashitaka unawakilishwa na mawakili wa Serikali Benard Kongora mashahidi tisa na Nassoro Katuga, washitakiwa walitetewa na Wakili Mohamed Tibanyendera na Hamidu Ubaidi ambaye baadaye alijitoa katika kesi hiyo kwa madai kuwa hapati muda wa kuzungumza na wateja wake.
Inadaiwa Februari 15, mwaka huu katika Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, washitakiwa walikula njama ya kutenda kosa na kukusanyika pasipo uhalali, jambo lililosababisha uvunjifu wa amani.
Katika mashitaka mengine, wafuasi hao wanadaiwa kuwa siku hiyo walishiriki kufanya vurugu na kukaidi amri ya Polisi iliyowazuia kuandamana.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item