PAPA AAHIDI KUPUNGUZA MADARAKA VATICAN...
https://roztoday.blogspot.com/2013/03/papa-aahidi-kupunguza-madaraka-vatican.html
Papa Francis (katikati) akiwa na baadhi ya makardinali. |
Papa Francis I amesimikwa rasmi na kutoa mwito wa wanyonge kulindwa sambamba na kuhifadhi mazingira, akisema vinginevyo kifo na uharibifu havitaepukika.
Akihutubia takriban watu 200,000 na viongozi wengi wa kigeni waliokusanyika katika viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Petro jana, Papa huyo Muajentina alitoa ujumbe wake ule ule alioutoa tangu anachaguliwa na makadinali Jumatano iliyopita, kwamba dhamira ya Kanisa ni kulinda masikini na wanyonge.
Pamoja na ujumbe huo, Misa hiyo iliyofanyika katika ngazi za Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,haikuwa ndefu kama ilivyokuwa ya mtangulizi wake Benedict, aliposimikwa rasmi mwaka 2005.
Dhamira ya Kanisa “inamaanisha kuheshimu kila kiumbe cha Mungu na kuheshimu mazingira tunamoishi. Ina maana kulinda watu, kuonesha upendo kwa kila mmoja, hususan watoto, wazee, wenye mahitaji na ambao tumekuwa tukiwafikiria mwisho,” alisema katika ujumbe wake.
Francis, ambaye awali alikuwa akijulikana kama Kardinali Jorge Bergoglio wa Argentina, alichukua jina lake kwa heshima ya Mtakatifu Francis wa Assisi, ambaye ni alama ya umasikini, ukawaida, kujitolea na kupenda asilia.
Alisema kila binadamu wanaposhindwa kujali mazingira na mwenzake, “Njia inafunguka kwa uharibifu na nyoyo zinakuwa nzito. Kwa bahati mbaya kila kipindi katika historia kuna akina Herode wanaopanga kifo, wanaosababisha ghasia na kutibua utulivu wa wanaume na wanawake.”
Ukawaida wa Francis, Papa wa kwanza Mjesuiti, umeleta matumaini ya mabadiliko na kuzaliwa upya kwa Kanisa lililokuwa limegubikwa na matatizo ya kidunia.
“Ni mtu wa kawaida, mnyenyekevu, si sawa na mapapa wasioguswa, anaonekana kama mtu ambaye watu wa kawaida kabisa wanaweza kumfikia,” alisema mmoja wa watu waliokusanyika katika kundi lile, mtaalamu wa umeme kutoka Argentina, Cirigliano Valetin (51), ambaye anafanya kazi Kusini mwa Italia.
Francis anarithi Kanisa lililogubikwa na kashfa juu ya mapadri kudhalilisha watoto na kuvuja kwa nyaraka za siri zikidai kuwapo kwa rushwa na upinzani kati ya makardinali ndani ya Kanisa na utawala wa Kanisa au Curia.
Pia amekuwa akituhumiwa na baadhi ya wakosoaji nchini Argentina kwa kushindwa kuchukua hatua za kutosha kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu chini ya utawala wa kijeshi wakati wa “vita chafu” mwaka 1976-1983 wakati watu 30,000 wa mrengo wa kushoto walipotekwa nyara na kuuawa. Vatican imeshakanusha tuhuma hizo.
Katika mahubiri yake, Papa huyo mpya alitaka viongozi wa dunia kuwa “walinzi wa kila mtu na wa mazingira … Tusisahau kwamba chuki, wivu na majivuno, vinaharibu maisha yetu. Kuwa walinzi, pia kunamaanisha kuchunga hasira dhidi ya nyoyo zetu.”
Kabla ya Misa hiyo, Papa alizuru viwanja vya Mtakatifu Petro, ambavyo vilifurika watu wakipepea bendera, akiwa ndani ya gari la wazi aina ya Jeep, akikwepa kutumia gari la upapa lisilopenywa risasi ambalo mara nyingi lilitumiwa na Benedict.
Alisimama mara kwa mara kusalimia waliokuwa wamejipanga kwenye uwanja huo, akibusu watoto na wakati mmoja alishuka kubariki mlemavu.
Katika Misa hiyo alivalia mavazi rasmi meupe, yakinakshiwa na mistari ya dhahabu na kahawia na viatu vyeusi, tofauti na vyekundu vya kifahari ambavyo vilikuwa kama alama ya Benedict.
Sherehe hiyo, iliyoendeshwa kutoka kwenye altare katika ngazi za kuingilia kanisani, ilifupishwa hadi saa mbili kutoka tatu kama ilivyokuwa mwaka 2005 wakati Benedict akianza upapa.
Baada ya Misa hiyo, mamia ya mapadri, walijifunika miavuli kujizuia jua katika eneo hilo lililonakshiwa rangi za njano na nyeupe, waligawa kumunio kwa umati huo huku Francis akiwaangalia akiwa kwenye kiti chake kwenye altare.
Kabla ya Misa hiyo, Francis alivikwa pete yake mpya iliyopakwa dhahabu na stola ambayo huvaliwa shingoni, ambayo usiku kucha ililala kwenye kaburi la Mtakatifu Petro katika altare ya Kanisa.
Alitoka nje ya Kanisa akiwa kwenye mstari akifuatiwa na makardinali huku wakiimba litania kutoa mwito wa kuungwa mkono kwa Papa mpya pamoja na watakatifu, wakiwamo mapapa kadhaa waliotangulia.
Watu wengi miongoni mwa waliohudhuria Misa ile walisema wana matumaini makubwa na unyenyekevu wa kipapa alionao Francis, ambaye kama Mjesuiti amechagua kushughulikia umasikini na kusema atawaangalia zaidi watu wa chini.
“Mtazamo wangu wa kwanza ni kwamba Papa huyu ni mnyenyekevu sana, na amelichukulia Kanisa kwa moyo wa dhati,” alisema Issac Adroamabe kutoka Arua, Uganda, ambaye anasomea upadri Roma.
“Nadhani atatimiza ahadi zake, ataongoza Kanisa akifuata misingi ya Mtakatifu Francis, unaweza kuona mwenyewe kuwa ni Papa anayejishusha, anayechanganyika na watu.”
Vigogo sita wa kimataifa, Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden, Rais wa Argentina, Cristina Fernandez, viongozi wengine pamoja na wakuu wa dini na madhehebu mbalimbali duniani walikuwa miongoni mwa wajumbe waliokaa kwenye ngazi za Kanisa hilo jana.
Miongoni mwao alikuwa Kiongozi wa Mtaguso wa Kanisa Bartholomew kutoka Istanbul, kwa mara ya kwanza kiongozi wa kiroho wa Wakristo wa madhehebu ya Orthodox alihudhuria Misa ya usimikwaji wa Papa wa kikatoliki tangu Mfarakano Mkuu kati ya Ukristo wa Magharibi na Mashariki mwaka 1054.
Katika siku sita tangu achaguliwe, Papa amekuwa akijiita Askofu Mkuu wa Roma, nafasi ambayo inaendana na madaraka yake na alipata kugusia mipango yake ya kupunguza madaraka ya Vatican na kuongoza kwa kushauriana na maaskofu wengine. Alitarajiwa jana kupokea viongozi wa kisiasa katika Kanisa hilo baada ya Misa.
Francis alikumbana na changamoto yake ya kwanza ya upapa juzi pale, Rais wa Argentina Fernandez alipomwomba aisaidie nchi yake katika mgogoro na Uingereza, kuhusu visiwa vya Falkland vilivyo Kusini mwa Bahari ya Atlantic. Msemaji wa Vatican hakuwa na la kusema kuhusu ombi hilo.
Pia alitarajiwa kukutana na kiongozi mashuhuri kimataifa, Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ambaye amezuiwa kusafiri na Umoja wa Ulaya (EU) tangu mwaka 2002 kwa madai ya kufanya udanganyifu katika uchaguzi na kukiuka haki za binadamu. Vatican si sehemu ya EU, hivyo haiwezi kumzuia Mugabe kusafiri.
Juzi Vatican ilizindua alama maalumu ya Papa; ngao ambayo inafanana na aliyokuwa akiitumia akiwa Askofu Mkuu wa Buenos Aires, ikiwa na michoro inayowawakilisha Yesu, Maria na Joseph.
Alama za upapa zimeongezwa nyuma yake, ikiwa ni pamoja na funguo mbili ambazo zinamaanisha aya kwenye Biblia, ambamo Yesu alimwambia Mtakatifu Petro atampa “funguo za ufalme” wa Mbingu.