WAISLAMU WAENDESHA SALA TANO NDANI YA KANISA...

Mchungaji Isaac Poobalan (kulia) na Imamu Mkuu Ahmed Megharbi wakiwa ndani ya kanisa hilo.
Kanisa la Kiskochi limekuwa la kwanza katika Uingereza kuchangia majengo yange na waumini wa Kiislamu.

Kanisa hilo la St John’s Episcopal la mjini Aberdeen sasa linakaribisha maelfu ya Waislamu kusali mara tano kwa siku katika majengo yao kufuatia Msikiti wa jirani kuwa mdogo mno hivyo kulazimisha waumini wake kusali wakiwa nje.
Mkuu wa kanisa la St John's, Mchungaji Isaac Poobalan, amekabidhi sehemu ya ukumbi wa kanisa hilo kwa Imamu Mkuu Ahmed Megharbi na imamu huyo akaongoza sala ndani ya kanisa dogo.
Mchungaji Poobalan alisema jana kwamba hawezi kuwa mkweli katika imani yake kama hatoi msaada.
Alisema: "Kusali si makosa kabisa. Kazi yangu ni kuhamasisha watu kusali.
"Msikiti huo ulifurika waumini wakati huo, kulikuwa na watu nje wakisali huku wakinyeshewa mvua.
"Nilifahamu nisingeweza kuruhusu hili litokee -  sababu ningekuwa natelekeza kile Biblia inachotufundisha kuhusu namna tunavyowatendea jirani zetu.
"Nilipozungumza na watu katika kanisa kuhusu hali hiyo, mmoja aliniambia hilo sio tatizo letu, lakini nilikuwa nimeshuhudia kwa macho yangu mwenyewe, hivyo lilikuwa tatizo.
"Nilipoongea na Imamu kulikuwa na kusita kwa upande wao, sababu hii haikuwahi kutokea hapo kabla.
"Lakini walikubaliana na ofa yetu na ukawa ushirikiano chanya.
Mchungaji Poobalan, mwenye miaka 50, alisema kuwa amezingirwa na Waislamu wakati akikua nchini India kulisaidia kuvunja mgawanyiko kwa waumini wa dini mbili na kuweza kusali pamoja mjini Aberdeen.
Shekhe Ahmed Megharbi wa Msikiti wa Masjid Syed Shah Mustafa Jame alisema: "Kilichotokea hapa ni maalumu na hakutakuwa na tatizo kurudia hili katika nchi nzima.
"Uhusiano huu ni wa kirafiki na kuheshimika."
St John's ni sehemu ya Kanisa la Scottish Episcopal, ambalo ni sehemu ya Umoja wa Anglican na tofauti kutoka Kanisa la Kiprotestanti la Scotland.
Askofu wa Aberdeen na Orkney, Mchungaji Robert Gillies alisema kwamba uhusiano huu unaweza kuwa mwanzo wa mabadiliko katika nguvu kati ya imani mbili.
Askofu Gillies alisema: "Itakuwa vema kufikiri tunaweza kubadili dunia.
"Wengi wetu wakati wote tunafikiri hatuwezi usijisumbue.
"Lakini wakati mwingine, mtu anamtazamo tunaweza kufanya kitu fulani chenye mtazamo mpana kutoka kiwango cha chini.
"Hicho ndicho kilichotokea kati ya St John's na msikiti mwanzoni.
"Kila mtu anaweza kufanya kitu fulani mahali pake na kama zaidi tulitakiwa kufanya hivyo basi kitu kikubwa lazima kianze kutokea dunia nzima."
Dk Gillies alisema kwamba 'macho ya dunia' sasa yalikuwa yakiangazia imani hizo mbili zilizowakilishwa ndani ya jengo moja kwenye Crown Terrace mjini humo.
Japo kanisa la Kikristo linamwamini Yesu kama mwana wa Mungu, imani ya Waislamu inamtazama kama Mtume.
Hata pamoja na tofauti kama hizi, kunaweza kuwa na kuheshimiana kwa pande mbili, alisema Dk Gillies.
Uhusiano kati ya msikiti na St John's umeendelezwa kwa zaidi ya miaka michache iliyopita.
Sherehe za Krismasi mwaka 2010 wote walifungua milango yao kwa ajili ya sala, chakula na kushirikiana.
Mwaka 2011, kanisa hilo na msikiti walishirikiana kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 10 ya shambulio la kigaidi la Septemba 11 lililotokea nchini Marekani.
Maandiko yalisomwa kutoka kote kwenye Biblia na Kuran tukufu kuwakumbuka wote waliokufa.
Kumekuwa na matukio ya Wakristo kuruhusu Waislamu kusali kwenye makanisa yao katika sehemu za Marekani.
Mwaka 2011, makanisa mawili mjini Florida yalishutumiwa kwa kuyafunguliwa milango makundi ya Waislamu.
Lakini viongozi wa Kanisa wanaamini uamuzi huo mjini Aberdeen ni wa kwanza kwa Uingereza.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item