WALIOGOMA BBC KUREJEA ENDAPO NELSON MANDELA ATAFARIKI DUNIA...

Waandishi na mafundi wa BBC wakitoka ofisini katika kutekeleza mgomo wao.
Viongozi wa chama wamesema wafanyakazi wa BBC waliogoma wanaweza kurejea kazini kwa ajili ya tukio la kifo cha Nelson Mandela - lakini wakasisitiza kwa kifo cha Baroness Thatcher hawawezi kuchukua hatua kama hiyo.

Wakati ilipobainika kwamba Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, amelazwa hospitali, viongozi wa chama wakaweka wazi kwamba mgomo ungeahirishwa kwa ajili ya tukio la kifo chake 'kwa ajili ya habari za BBC kuripoti stori hiyo pekee'.
Lakini swali endapo hatua kama hiyo itachukuliwa kwa tukio la kifo cha Baroness Thatcher - kudra za chama cha harakati za wafanyakazi katika miaka ya 1980 - haikufikiwa kwa sawa na huo.
Waandishi na mafundi walifanya mgomo wa masaa 12 mchana wa juzi katikati ya upunguzwaji wafanyakazi, kurundikiwa kazi na madai ya uonevu kwenye shirika hilo.
Chama cha Taifa cha Waandishi wa Habari (NUJ) na Bectu vyote vimesema hawajali hatua hiyo itakavyokuwa katika tukio la kifo cha waziri mkuu huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 87.
"Mandela, na historia yake katika vyama vya wafanyakazi, ni mtu muhimu sana kwa kila mmoja," alisema msemaji wa NUJ.
Msemaji wa BBC alizungumzia msimamo wa chama hicho kuelekea mgomo wa juzi kufuatia hali ya Mandela: "Tunalipokea tangazo hili na ni shukrani kwa sura ya wafanyakazi wa BBC."
Mgomo huo, ambao uliendelea hadi usiku wa manane, umepelekea kufutwa kwa vipindi vya Newsnight cha  BBC 2, Kipindi cha PM cha Radio 4 na World Tonight.
Moja ya sababu za mgomo huo ni madai kwamba wafanyakazi walikuwa 'wakiteswa' kufanya kazi zaidi kutokana na kupunguzwa kwa wafanyakazi.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item