BINTI WA MIAKA MITANO MAHUTUTI BAADA YA KUFUNGIWA SIKU NNE NA KUBAKWA...
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/binti-wa-miaka-mitano-mahututi-baada-ya.html
Mtoto huyo (akiwa kafunikwa shuka) akiwahishwa hospitalini kwa matibabu. |
Binti mwenye miaka mitano yu mahututi baada ya kubakwa na jirani yake huko Gandhi Nagar, mashariki mwa Delhi, ambako alishikiliwa mateka kwa siku nne.
Mtoto huyo ambaye alitekwa nyara wakati akicheza nje ya nyumba yao na kufungiwa kwenye ghorofa la jirani yao kwa siku kadhaa kabla mtu mmoja kumsikia akilia kuomba msaada.
Madaktari waliripoti kugundua 'vitu vigeni' ndani ya viungo vyake vya uzazi huku taarifa zaidi kuhusu mateso yake zikianza kuanikwa hadharani.
Binti huyo wa miaka mitano alitoweka kutoka nyumbani kwao Jumatatu na kupatikana Alhamisi usiku kwa msaada wa waokoaji, waliogutushwa na kelele zake, ndani ya nyumba ya mwanaume ambaye anaishi kwenye jengo hilo pamoja Jirani huyona familia ya mtoto huyo.
Jirani huyo anaaminika kuwa alimbaka mtoto huyo kwa kurudiarudia kuharibu viungo vyake vya uzazi na kujaribu kumnyonga.
Madaktari wa Swami Dayanand mjini Delhi walisema waligundua vitu vigeni ndani ya mtoto huyo, ikiwamo chupa ya milimita 200 na vipande vya mshumaa uliovunjika.
Pia alipata majeraha na michubuko kifuani kwake, midomoni na mapajani.
Dk R.K. Bansal ambaye alimchunguza mtoto huyo alisema ilikuwa 'moja ya matukio mabaya kabisa' aliyowahi kushuhudia, na kwamba masaa 48 yajayo yatakuwa ya kipekee katika kubaini nafasi yake ya kuishi.
"Alishikwa na hofu na kutojiamini," alieleza. "Mwanzoni, hakuturuhusu kuendelea na uchunguzi kutokana na kuwa katika maumivu makali mno."
Hili ni tukio la tatu la ubakaji kudaiwa kutokea ndani ya mwezi huu katika eneo la mji wa Delhi. Mapema wiki hii mtoto wa miaka 10 alidaiwa kubakwa kwenye basi mbele ya dereva, pia katika kesi hii jirani, alimrubuni atoroke nyumbani kwao.
Wiki iliyopita msichana mwingine, pia mwenye miaka 10, alidaiwa kubakwa na jirani yake na kisha kufungiwa selo na polisi baada ya familia yake kujaribu kuripoti uhalifu huo.
Kesi hiyo imeibua maandamano makubwa nje ya hospitali ya Swami Dayanand huku mamia wakishutumu vitendo vya watuhumiwa na kuishutumu serikali kwa kutotoa uangalizi mzuri na polisi kwa kutoshughulikia ripoti za wazazi za kupotelewa watoto wao.
Familia ya binti huyo inadai polisi hao walijaribu kuwahonga Pauni 24 kuwanyamazisha baada ya binti yao kuokolewa na kugoma kuichukulia kama kesi ya ubakaji.
"Alikwenda nje kucheza ndipo akatekwa nyara. Mwanaume huyo kisha akamfungia kwenye chumba chake na kumbaka. Ninataka haki kutoka kwa serikali," mama wa binti huyo alieleza.
Jana, wakati binti huyo akihamishiwa All India Institute of Medical Sciences ili kuweza kupatiwa uangalizi mzuri zaidi, Polisi wa mjini Delhi waliripoti kumtambua mtuhumiwa huyo wa ubakaji.
"Mtuhumiwa ameshatambuliwa na timu tayari inakaribia kumkamata," Kamishna wa Polisi Delhi Neeraj Kumar alieleza.