KOCHA WA VIUNGO ALIYEDUMU MIAKA 19 ATIMULIWA SHULE KATOLIKI KWA USAGAJI...
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/kocha-wa-viungo-aliyedumu-miaka-19.html
Carla Hale. |
Kocha wa elimu ya viungo huko Columbus, Ohio amepatwa na mshituko baada ya shule Katoliki ambako amefundisha kwa miaka 19 kumtimua kwa kuwa msagaji.
Carla Hale, mwenye miaka 57, kutoka Powell, alipewa onyo siku za mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya kumbukumbu ya marehemu mama yake mnamo Februari likielezea mahusiano ya Carla na mwanamke aliyetajwa kwa jina la Julie.
Wakati mzazi wa mmoja wa wanafunzi aliposikia tangazo hilo na kulalamika kwa mamlaka za shule, Carla aliondoshwa papohapo kwenye viwanja kwamba alikuwa 'amekiuka sera ya kiroho ya shule hiyo.'
Huku akibubujikwa machozi, Carla alieleza: "Bishop Watterson ni sehemu ya kustaajabisha kuwepo. Wafanyakazi, mazingira..."
Baada ya kipindi kirefu cha kufanya kazi katika shule hiyo, hakuweza kuamini masikio yake pale alipooneshwa rambirambi hiyo na kuelezwa kwamba mahusiano yake yameshika ahadi kwa sera ya kidayosisi.
"Hakika ilinishitua kabisa," Carla alisema. "Namaanisha, nafikiri ilikuwa moja kati ya yote ambako kila kitu kilikaushwa kutoka kwangu."
Carla, ambaye alikiri mara zote kuweka maisha yake binafsi kuwa siri kazini, alitumiwa barua ikielezea taratibu za Dayosisi hiyo.
"Katika kuweka thamani za kiimani zinazosukumwa na mafundisho ya Yesu, itikadi za Kanisa Katoliki, na sera hizo na taratibu za dayosisi na shule, watu wa shule Katoliki wanatarajiwa kuwa mfano wa tabia ya kiroho na weledi," inasema barua hiyo.
Barua hiyo iliendelea kusema kwamba: "Mahusiano yako ya jinsia moja yanakiuka sheria za kiroho za Kanisa Katoliki, katika Makubaliano ya COACE Kipengele 20.3. Kutokana na hilo, mkataba wako na Shule ya Sekondari ya Juu ya Bishop Watterson umevunjwa kuanzia Alhamisi ya Machi 28, 2013."
Katika ofa ya haraka ya fidia, Carla amepewa barua ya mapendekezo na nafasi ya kubakiwa na bima yake ya afya kwa kipindi cha hadi mwaka mmoja.