MWANAMKE AKAMATWA NA COCAINE ZA SHILINGI MILIONI 28 SEHEMU ZA SIRI...
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/mwanamke-akamatwa-na-cocaine-za.html
Mwanamke mmoja amekamatwa akiwa na dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya Pauni za Uingereza 100,000 (zaidi ya Shilingi milioni 28 za Tanzania) alizokuwa ameficha katika nguo zake za ndani kwenye ndege alipokuwa akirejea nchini Uingereza.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Argentina alisema: "Dawa hizo za kulevya zilikuwa zimefungwa vizuri sambamba kufuatisha shepu lake."
Alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ezeiza na amewekwa rumande katika gereza la wanawake mjini Buenos Aires.
Tayari alikuwa chini ya uchunguzi wa polisi wakati wa kukamatwa kwake.
Polisi walisema kwamba kwa sasa wanajaribu kutambua genge ambalo limemlipa mwanamke huyo kusafirisha dawa hizo za kulevya kwenda nchini Uingereza.
Wachunguzi walinyang'anya gramu hizo 850 za cocaine alizokuwa amebeba.
Msemaji huyo aliongeza: "Hii si mara ya kwanza kumzuia mwanamke akiwa amebeba dawa za kulevya zilizofichwa katika sehemu zake za siro."
"Cocaine hizo alizokuwa amebeba zinakadiriwa kuwa na thamani takribani Pauni 100,000 nchini Uingereza endapo zingekuwa zimeuzwa katika kiasi kidogo kidogo."