UPEPO MKALI WASABABISHA NDEGE KUTUA UPANDE UPANDE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/upepo-mkali-wasababisha-ndege-kutua.html
Hili ni tukio la kusitisha mapigo ya moyo wakati ndege ilipotua kuelekea upande mwingine huku rubani akipambana na upepo mkali ulioikumba Uingereza jana.
Ndege hiyo ya Ryanair kwenye Uwanja wa Ndege wa Leeds ilinaswa kwenye picha ikitua kinyume cha ilivyozoeleka, na kusababisha moshi mkubwa kufoka kutoka kwenye magurudumu yake wakati ikigusa chini kwenye njia hiyo ya kuruka/kutua.
Ndege nyingine zilihangaika kuruka sababu ya hali mbaya ya hewa.
Upepo mkali wa kasi ya maili 72 kwa saa ulirekodiwa eneo la jirani na Emley Moor, karibu na Huddersfield, West Yorkshire, katika saa za mapema wakati kaskazini ya Uingereza ilikumbwa na upepo mkali.
Msemaji wa uwanja huo wa ndege alisema kulikuwa na uchelewaji wa ndege zilizokuwa zikiruka kwenda Faro, Alicante, Southampton, Barcelona, Brussels na Southampton sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Ndege zililazimika kusubiri hadi kasi ya upepo ilipopungua na ikawa salama kuruka kabla ya kuhakikishiwa kufanya hivyo kama tahadhari.