WAFUNGA NDOA SAA CHACHE BAADA YA MILIPUKO YA MARATHONI ZA BOSTON...
https://roztoday.blogspot.com/2013/04/wafunga-ndoa-saa-chache-baada-ya.html
Robert Watling (kulia) na Kelli Johnston wakifungishwa ndoa. |
Huku ugaidi ukichomoza katika milipuko mikubwa ya mabomu kwenye marathoni, kona moja ya jiji ilishuhudia tukio la furaha.
Wakimbiaji wa marathoni Robert Watling na Kelli Johnston, wote wana umri wa miaka 38, walifunga ndoa kwenye bustani ya jijini humo chini ya kipindi cha masaa manne baada ya kumaliza mbio zao, huku magari ya wagonjwa yakiendelea kutimua vumbi kwenda na kurudi eneo la tukio la milipuko miwili kwenye eneo la karibu na mstari wa kumaliza mbio.
Bwana harusi na Bi harusi, ambao wote walivalia nguo za michezo na mdali zao za marathoni huku wakibadilishana viapo juzi, waligoma kuacha milipuko hiyo ya mabomu izuie ndoa yao kusonga mbele.
Bi harusi huyo alitangaza kwenye mtandao wa Facebook kwamba harusi hiyo iliendelea, akiongeza: "Moyo wangu uko pamoja na wote waliouawa na kujeruhiwa hapa leo katika tukio hili Boston."
Posti yake pia ilisema: "Robert Allan Watling na mimi tumemaliza vema marathoni hizo kabla ya mabomu na kufunga ndoa kwenye bustani hiyo!! Mvinyo kwa wote!"
Wakimbiaji hao waliojitenga - ambao walishiriki mbio za Kilomita 5 pamoja katika siku yao ya kwanza - walikuwa wamepanga sherehe hiyo tangu Watling alipochombeza swali hilo baada ya kuwa wamemaliza Marathoni hizo za Chicago.
Katika kuendana na kaulimbiu hiyo, waliamua kufunga ndoa katika foleni ya picha Boston Common baada ya kumaliza Marathoni za Boston.
Kelli na Robert wote walikuwa wamevuka mstari wa kumaliza kabla ya mabomu kulipuka yakiachiana muda wa sekunde 12 katika Mtaa wa Boylston majira ya Saa 8:50 mchana.
Katika milipuko hiyo iliyokatisha maisha ya watu watatu, akiwamo mtoto wa miaka minane, Martin Richard, na kujeruhi watu 144. Kati ya wote waliojeruhiwa, 17 wako mahututi.
Licha ya hali mbaya eneo la tukio, wawili hao walichagua kuendelea na sherehe yao majira ya Saa 12:20 jioni katika bustani hiyo.
Walishuhudiwa na mkusanyiko mdogo wa wanafamilia, imeripotiwa.
Robert alisema kabla ya mbio hizo kwamba watu walifikiwa walikuwa 'vichaa' kufunga ndoa mara tu baada ya kuwa wamekimbia kwenye marathoni.
Watling alikuwa amemvisha pete ya uchumba wakati akikimbia Marathoni za Chicago, lakini alisubiri hadi saa chache baada ya mbio kuoa kwa ushauri wa marafiki zake.
"Marafiki zangu wachache walishinikiza kwa nguvu zote kwamba nisubiri hadi baadaye jioni ya siku hiyo, huku wanawake walitaka kushuhudia uhondo katika tukio hilo," alisema wiki iliyopita.