CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2013/06/cheka-taratibu_10.html
Mwalimu mgeni aliingia darasani kwa mara ya kwanza na kuchora moyo ubaoni. Kwa vile hakuwa mchoraji mzuri ule moyo ukaonekana ovyo. Kwa kujiamini akawauliza wanafunzi:
"Nimechora nini?" Mwanafunzi wa kwanza akajibu: "Makalioooo!" Mwanafunzi wa pili akajibu: "Umechora makalio mwalimu!" Mwanafunzi wa tatu akajibu: "Hayo ni makalio kabisaa!" Mwalimu kwa hasira akaenda kushitaki kwa mkuu wa shule kwa madai wanafunzi wanafanya mzaha. Mkuu wa shule akaingia darasani na kuwaonya wanafunzi waache mzaha kisha akatazama ubaoni na kusema kwa ukali: "Enhe, nitajieni aliyechora makalio ubaoni?" Duh...
