MFANYAKAZI WA SHIRIKA LA NDEGE AGOMA KULA KUDAI MALIMBIKIZO YA MSHAHARA WAKE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/06/mfanyakazi-wa-shirika-la-ndege-agoma.html
![]() |
| KUSHOTO: Kaunta ya Ofisi za Shirika hilo ikiwa imefungwa. KULIA: Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Sanjay Agarwal. |
Mfanyakazi wa shirika la ndege lenye makao yake Mumbai ameingia kwenye mgomo wa kula kufuatia kutolipwa mshahara wake kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Wafanyakazi 70 wa Shirika la Kingfisher Airlines, ambalo lilisitisha shughuli zake Oktoba 2012 sababu ya matatizo ya kifedha, wanaandamana nje ya makao makuu ya kampuni hiyo mjini Mumbai, kwa mujibu wa Shirika la Habari la Bloomberg.
Wafanyakazi hawajalipwa tangu Agosti 2012, na wanasemekana kuwa wamechanganyikiwa baada ya kuomba msaada wa Serikali.
Imeripotiwa kwamba mgomo wa kula hauna mwisho na hautasitishwa hadi malipo ya haraka ya malimbikizo ya mishahara yamefanyika.
Kingfisher Airlines lilisimamishwa Oktoba 2012 baada ya kushindwa kushindwa kujibu maswali ya mamlaka kuhusu hali yake ya kifedha na usalama.
Mwaka 2012, kampuni hiyo ilikuwa katika deni la Pauni za Uingereza 641,000,000 kwa taasisi mbalimbali 17. Sehemu ya ndege zake zililazimika kusitisha shughuli na wafanyakazi kuingia katika mgomo.
Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Sanjay Agarwal anaaminika kuwapo ofisini akijaribu kushawishi wafanyakazi kumaliza mgomo wao, kwa mujibu wa TravelMole.
Ahadi za kuanza upya shughuli zimekuwa zikitolewa tangu Februari na mipango ya kulifufua shirika hilo iliwasilishwa kwa mamlaka za India mwezi Aprili.
