CHEKA TARATIBU...

https://roztoday.blogspot.com/2013/06/cheka-taratibu_26.html
Daktari hospitali moja ya vichaa kawapa vipande vya sabuni wagonjwa wake wawasiliane na wapenzi wao.
Huku wote wakitumia vipande hivyo kama simu za mkononi, kichaa mmoja akajibanza kimya pembeni huku kashikilia kipande chake cha sabuni mkononi. Daktari akafurahi na kuamini atakuwa amepona. Daktari akamfuata na kumuuliza kwanini hafanyi kama wenzake? Kichaa akajibu: "Nasubiria usiku maana mtandao huu wanakata hela nyingi sana mchana! Duh...