MANDELA AFUMBUA MACHO NA KUTABASAMU ALIPOSIKIA ZIARA YA OBAMA AFRIKA KUSINI,,,

Mzee Nelson Mandela.
Mzee Nelson Mandela alifungua macho yake na kutabasamu pale alipoambiwa kuhusu ziara ijayo ya Barack Obama nchini Afrika Kusini, kwa mujibu wa binti yake.

Baba huyo wa taifa hilo mwenye miaka 94 yuko katika mbaya hospitalini mjini Pretoria, lakini licha ya hayo alimudu kuonesha furaha yake baada ya kusikia ziara ya Rais huyo wa Marekani.
Obama anaaminika kudhamiria kukutana na Mzee Mandela, lakini kutokana na kuelezwa hali tete ya kiongozi huyo wa Afrika hataweza kufanya hivyo isipokuwa kwa mwaliko wa familia ya Mandela.
Uwezekano huo ulionekana kuweza kutimia juzi baada ya binti wa Mandela, Zindzi kuelezea jinsi alivyomtaarifu baba yake kwamba Obama atatembelea Afrika Kusini.
Baada ya kumweleza "Obama anakuja," alisema, "Alifungua macho yake na kutabasamu."
Rais huyo wa Marekani alielekea Senegal jana na atawasili Afrika Kusini Ijumaa wakati wa ziara yake barani Afrika tangu ashike wadhifa huo.
Mzee Mandela amekuwa hospitalini akitibiwa maambuko kwenye mapafu tangu Juni 8, na mwishoni kwa wiki aliripotiwa kutoka 'hali mbaya' hadi 'mahututi'.
Juzi Askofu wa Cape Town alimfanyia maombi Rais huyo wa zamani baada ya kumtembelea hospitalini.
Thabo Makgoba alituma ujumbe katika mtandao wa Facebook akitaka kumpa moyo mke wa Mzee Mandela, Graca Machel, na wengine wanaompenda 'katika kipindi hiki kigumu cha kutazama na kusubiri'.
Ndugu wa karibu wa Mzee Mandela juzi walifanya mkutano wa dharura nyumbani kwa kiongozi huyo mpinga ubaguzi wa rangi huko Qunu, Mashariki mwa Cape.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item